Tishati iliowashangaza wengi mitandaoni

Tishati ya Balenciaga Haki miliki ya picha Balenciaga

Kampuni ya fesheni ya Balenciaga inauza tishati za wanaume kwa bei ya £935 ikiwa ni miongoni mwa mkusanyiko wa nguo zake zilizoundwa mwaka 2018

Kwa wengi sio bei iliowashangaza bali mtindo wa nguo ilivyotengezwa. Nguo hiyo ni tisheti ambayo ina shati lililotundikwa juu yake swala lilowawacha wengi vinywa wazi.

Kulingana na mtandao wa Balenciaga tishati hiyo inaweza kuvaliwa mara mbili na hivyobasi kuonekana kana kwamba imetundikwa katika mwili wa mtu. Watu wengi wameamua kutengeneza tishati zao zenye mtindo kama huo, kwa gharama ya chini.

Watu wamewachwa na maswali mengi yasio na majibu kuhusu ni kwa nini Balenciaga ilidhani ni wazo zuri.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii