Siku ya Kupinga Matumizi ya Tumbaku Duniani: Nchi gani huvuta sigara kwa kiasi kikubwa?

Woman smoking in cafe

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

One million French smokers have quit in a year amid anti-smoking measures

Ufaransa imeshuhudia kupungua kwa idadi ya watu wanaovuta sigara kila siku, mwaka 2016 mpaka 2017.

Hatahivyo, ingawa kumekuwa na sera za kuzuia matumizi ya tumbaku kwa kipindi cha karne kadhaa, idadi ya wavuta sigara duniani imeongezeka, utafiti uliofanyika mwaka jana umebainisha

Katika kuadhimisha upingaji wa matumizi ya tumbaku dunianu, tumeorodhesha nchi zinazovuta sigara kwa wingi, kwa mujibu wa shirika la afya duniani, WHO takwimu za kuanzia mwaka 2016

1) Kiribati

Kisiwa cha Kiribati kina idadi kubwa zaidi ya wavuta sigara, takriban theluthi mbili ya wanaume huvuta sigara na zaidi ya theluthi ya wanawake

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kisiwa cha Kiribati ina ushuru mdogo wa sigara

Idadi ya watu katika visiwa hivi vya Pacific ni103,000 pekee, visiwa hivi vina sera zisizo kali kuhusu tumbaku na ushuru kwa bidhaa za sigara ni mdogo

2) Montenegro

Ni nchi iliyo mashariki mwa Ulaya ina kiwango kikubwa cha uvutaji wa sigara barani Ulaya takribani 46%.

Nchi hii ina watu 633,000 na zaidi ya sigara 4,124 huvutwa na watu wazima kwa mwaka.

Ingawa kuvuta hadharani kumepigwa marufuku,watu wanaendelea kuvuta sigara kwenye Ofisi, migahawa, vilabu vya pombe na hata kwenye usafiri wa umma

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Zaidi ya 50% ya wanaume huvuta sigara nchini Ugiriki

3) Ugiriki

Ugiriki ni ya tatu kwa uvutaji sigara, zaidi ya nusu ya wanaume nchini humo huvuta sigara na wanawake 35%

Ingawa kumekuwa na sheria dhidi ya uvutaji wa sigara katika maeneo ya wazi tangu mwaka 2008,watu wanaonekana wakivuta sigara kila mahali.

Kuna sigara nyingi ambazo huingizwa nchini humo kinyume cha sheria, Kampuni inayofanya utafiti wa masuala ya masoko umebaini kuwa Athens huenda ikapoteza mapato kiasi cha Euro bilioni moja mwaka 2019

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Sigara nyingi zina gharama ya chini ya dola moja Timor Mashariki

4) Timor Mashariki

Timor Mashariki ni moja kati ya nchi zenye viwango vya juu vya uvutaji , asilimia 80 ya wanaume wanavuta sigara, idadi kubwa zaidi ulimwenguni

Asilimia 6 pekee ya wanawake nchini humo wanavuta sigara.

Katika taifa hili masikini ,Pakiti ya sigara huuzwa kwa gharama ya chini ya dola moja

Pakiti zote za sigara zina maandishi ya tahadhari lakini hizi hazina maana kwa kuwa karibu nusu ya watu nchini humo hawajui kusoma

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Soko la Sigara nchini Urusi lina thamani ya zaidi ya dola bilioni 22

5) Urusi

Urusi ni ya tano kwa uvutaji sigara, takriban asilimia 60 ya wanaume wenye zaidi ya umri wa miaka 15 wanavuta sigara na asilimia 23 ya wanawake.

Uvutaji sigara sehemu za kazi na kwenye usafiri wa Umma ni kinyume na sheria lakini matangazo ya tumbaku huchangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la uvutaji sigara.

Katika baadhi ya maduka, Pakiti za sigara zinaweza kununuliwa kwa gharama ya chini ya dola moja.

Soko la sigara nchini Urusi linakadiriwa kuwa zaidi ya dola bilioni 22.

Nchi zenye wavutaji wachache

Nchi ambazo huvuta sigara kwa kiasi kidogo ni Ghana, Ethiopia, Nigeria, Eritrea na Panama.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Uvutaji kwa wanawake hutazamwa kama jambo lisilo la maadili

Takribani ilimia 14 ya waafrika huvuta tumbaku kwa mujibu wa WHO, ndogo kuliko wastani wa dunia wa takriban asilimia 22.

Wanaume ni asilimia kati ya 70 na 80-uvutaji wa sigara kwa wanawake unaelezwa kutokana na hali ngumu ya kiuchumi

Uvutaji wa sigara kwa wanawake umeelzwa kuwa ni kinyume cha maadili

Ghana, Ethiopia na Nigeria ambao wamejiunga na mapambano ya WHO dhidi ya tumbaku umweweka mpango wa kudhibiti na kuwasaidia raia kufahamu madhara ya uvutaji.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Utafunaji wa Khat hufananishwa na unywaji wa kahawa chungu

The popularity of a rival stimulant - a leafy plant called Khat which is chewed widely in the Horn of Africa - may also explain low rates of smoking in this region.

Mmea uitwao Khat hutafunwa kwa kiasi kikubwa katika pembe ya Afrika, hii inaeleza ni kwa kiasi gani cha uvutaji kipo kwenye eneo hili.

WHO inakadiria kuwa watu milioni 10 hutafuna mmea wa Khat duniani.

Ingawa uvutaji wa sigara Afrika bado ni ndogo , kwa asilimia 13, Kiasi hiki ni kikubwa katika nchi zinazoendelea, kwa mujibu wa jarida la kitabibu la Lancet.

Uvutaji umekuwa ukipungua kwa nchi za magharibi kutokana na kuongezeka kwa sheria, ufuatiliaji na kodi, kwa hivi sasa soko la tumbaku limekuwa likiongezeka katika nchi zinazoendelea, hasa likiwavuta zaidi vijana.

Watumiaji wakubwa wa tumbaku.

Chanzo cha picha, Tiago_Fernandez

Maelezo ya picha,

Mwaka 2016,matumizi ya tumbaku nchini China yalianza kushuka kwa mara ya kwanza kwa kipindi cha miongo miwili

China ni mzalishaji mkubwa na mtumiaji wa tumbaku duniani, kwa mujibu wa WHO.

Kuna zadi ya wavutaji milioni 300 nchini China, karibu theluthi moja ya idadi ya watu duniani.

Wanawake

Nchi pekee yenye wavutaji sigara wa kike wengi kuliko wanaume nchini Denmark, asilimia 19.3 ya wanawake wanavuta , wanaume ni asilimia 18.9.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Idadi ya wanawake wanaovuta sigara uko juu nchini Denmark

Kwa hakika idadi kubwa ya wanawake wanaovuta wanapatikana barani Ulaya, ambapo kumekuwa na tofauti ndogo sana kati ya wavutaji wa kike na wa kiume.

Tumbaku huua zaidi ya watu milioni saba kila mwaka

Lakini zaidi ya vifo milioni sita vinatokana na matumizi ya moja kwa moja ya tumbaku

Kwa mujibu wa WHO, takriban 80% ya wavutaji bilioni 1.1 wanaishi kwenye nchi zenye uchumi wa kati na zenye vipato vidogo.

Soko la tumbaku duniani linakadiriwa kuwa na thamani ya dola bililioni 770