Je unajuwa ni kwa nini maiti hawazikwi kwa miezi au hata kwa miaka nchini Ghana?

Majeneza huagizwa kwa mtindo unaovutia Ghana

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Majeneza huagizwa kwa mtindo unaovutia Ghana

Wiki iliyopita kulikuwa na taarifa jinsi mazishi yanavyotekelezwa huko Ghana.

Mwili wa chifu aliyefariki miaka sita iliyopita ulikuwa kwenye hifadhi ya maiti kutokana na mzozo kwenye familia ya nani atakaye kuwa ''muombolezaji maalum.''

Lakini taarifa hiyo haishangazi kwani ni mazoea ya raia wa Ghana kuiacha miili ya wafu kwenye hifadhi ya maiti kwa muda mrefu ili kusuluhisha mizozo inayoibuka baada ya kifo chochote kinachotokea nchini humo.

Maelezo ya picha,

Raia wa Ghana wanasifika kwa mageneza yaliyobuniwa kwa miundo tofauti kama hili lililotengenezwa maalum kwa chifu.

Raia wa Ghana wanasifika kwa majeneza yaliyobuniwa kwa miundo tofauti kama hili lililotengenezwa maalum kwa chifu.

Utamaduni huu unaangaziwa na jamii inayotoka kusini mashariki, Ga.

Maonyesho ya majeneza yamefunguliwa rasmi ya Jack Bell Gallery huko London.

Mazishi yaliyoghali zaidi na yaliojaa mbwembwe na majeneza yaliotengenezwa kwa miundo tofauti yamehifadhiwa.

Mageneza ya kuvutia

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Raia wa Ghana wanafahamika kwa ubunifu wao wa majeneza.

Lakini jukumu la ''familia'' kwenye mazishi ni lipi

Unaweza kudhani kwamba unatambua nani hasa ni familia yako. Lakini kifo kinapotokea ,maelezo kuhusu familia hubadilika kabisa.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Raia wa Ghana akipinga ngoma wakati wa mazishi.

Ni familia tu, yaani jamaa zako wa upande uliko zaliwa ndio hutoa uamuzi wa nani atakaye kuwa muombolezi mkuu na vyeo vyote ambavyo hutokana na kifo.

'Familia hiyo' na muombolezaji mkuu wanaweza kuwa hawajazungumzi kwa muda wa zaidi ya miaka 30 na marehemu, lakini wanatambulika kumfahamu zaidi aliyefariki kuliko mpenzi wake na watoto.

Chanzo cha picha, Other

Maelezo ya picha,

Mfano wa geneza hili litengenezwa mwaka 1951 na seremala wawili , Kane Kwei na kakake Adjetei. Walitengeneza geneza hilo kwa bibi mwenye umri wa miaka 91 ambaye hakuwahi kusafiri kwa ndege lakini aliwaambia kwamba alitamani kusafiri kwa ndege.

Baada ya hapo ndipo mikutano isiyoisha hufuata inayoongozwa na 'familia', pale maneno ya mpenzi wa marehemu na watoto yanapuziliwa mbali.

Tena wiki kadhaa hutumika kuandika tangazo la kifo kwenye gazeti na ni kazi ngumu kuandika orodha ya waombolezaji kwa hadhi zao.

Kwa hivyo siku nyengine ukikutana na tangazo kama hilo kwenye gazeti la Ghana , ni heri uthamini kazi hiyo ya uandishi wa tangazo hilo ili kuhakikisha hakuna migogoro ya aina yoyote inatokea au hata migogoro ya hapo awali kuzuka upya.

Jukumu la kumchagua muombolezi mkuu ni gumu sana kwa sababu si yeye pekee ndiye anayetoa maagizo ya mazishi , yeye pia lazima awe mwanamume na si mwanamke, yeye ndio anayetoa uamuzi wa mwisho wa nani atakaye mrithi marehemu.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Miguu ya marehemu akiwa kwenye nyumba ya kuhifadhi maiti

Kwa wakati huo wote, mwili wa marehemu huhifadhiwa kwenye jokovu iwapo kutakuwepo na migogoro ya lini na wapi marehemu atakapo zikwa.

Si jambo la kushangaza kwamba mara nyingi watu hujipata kortini kwa makosa ya kumzuia mtu kuuondoa mwili wa marehemu.

Kwa mara nyingi , ucheleweshwaji wa mazishi hautokani na mizozo.

Sisi huchukulia maanani kumpatia marehemu mazishi ya hali ya juu.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Densi na nyimbo ni sehemu ya mazishi nchini Ghana

Huwa tunaifanyia marekebisho nyumba ya marehemu alipofia au hata kumjengea nyumba mpya ili kukidhi kiwango cha mazishi.

Hilo huchua muda.

Iwapo mtu anawakata wageni mashuhuri kwenye mazishi hayo , hapo basi tarehe maalum inastahili kubuniwa kulingana na wageni hao.

Na hilo pia huchukua wakati mwingi.

Katika mazishi ya mfanyibiashara na mwanasiasa maarufu ,Nana Akenten Appiah-Menka.

Chanzo cha picha, Other

Maelezo ya picha,

Jeneza hili maalum linaaminika kutoka huko Teshi, jamii ya wavuvi iliyo nje kidogo ya mji mkuu wa Accra. Mvuvi angezikwa kwenye geneza lenye umbo la samaki.

Kitabu cha maelezo ya mazishi kilikuwa na kurasa 226 ya picha zake na risala za rambirambi kuhusiana na maisha yake aliyoishi ya miaka 84.

Pia hilo huchukua muda kukusanya hayo yote.