Unyanyasaji wa watoto washuhudiwa Tanzania Uganda na DRC

Data inaashiria wasichana ndio walio katika hatari zaidi ya kunyanyaswa

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Data inaashiria wasichana ndio walio katika hatari zaidi ya kunyanyaswa

Tanzania, Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na Rwanda ni miongoni mwa nchi 11 ambapo unyanyasaji wa watoto kingono unashuhudiwa kwa zaidi ya asilimia 10 miongoni mwa watoto walio na umri wa miaka 15- 19 kwa mujibu wa ripoti mpya ya shirika la kutetea haki za watoto Save the Children.

Ripoti hiyo inakuja huku maadhimishio ya siku ya watoto duniani ikiwadia Juni mosi hapo Kesho Ijumaa.

Zaidi ya nusu ya watoto duniani wamo katika hatari ya kukabiliwa na unyanyasaji dhidi ya wasichana, umaskini pamoja na mizozo.

Licha ya kuwa wavulana na wasichana huenda wanaweza kulengwa katika unyanyasaji wa kingono, data inaashiria wasichana ndio walio katika hatari zaidi.

Zaidi ya mtoto mmoja kati ya 10 wamewahi kulazimishwa kushiriki ngono au vitendo vya ngono vya kulazimishwa kwa wakati mmoja maishani mwao.

Nchi zimeorodheshwa kwa alama kulingana na ni kwa kiasi gani watoto wanafariki, kukabiliwa na utapia mlo, wanakosa elimu na kulazimishwa katika ndoa za utotoni, kuzaa na kutumikishwa katika kila nchi.

Katika orodha inayojumuisha mataifa 175 duniani Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ndiyo iliyokuwa chini zaidi katika orodha hiyo miongoni mwa ataifa ya Afrika mashariki katika nafasi ya 166 ya matafa ambapo watoto hawapat fursa ya kukuwa kama watot wa kawaida.

Hii ni kutokana na mizozo inayosuhhudiwa nchini humo umaskini uliokithiri na unyanyasaji miongoni mwa watoto wa kisichana nchini.

Somalia ipo katika nafasi ya 170 ikifuatwa nyuma na Sudana kusini katika nafasi ya 171.

Shirika la Save the Children linasema licha ya kwamba hali imeimarika duniani ikilinganishwa na mwaka jana, hatua haipigwi kwa kasi inayostahili.

Ripoti hiyo inaeleza kwamba hali hii inatokana na kwamba watoto hao wanaishi katika maeneo yanayogubikwa na umaskini mizozo na katika maenoe ambapo unyanyasaji wa wanawake ni jambo la kawaida.

"Kutokana na kuwa wao ni watoto na maeneo wanayoishi, wamo katika hatari ya kunyimwa kuwa watoto na mustakabli wao," ripoti imesema.

Maelezo ya video,

Wasichana nchini Ghana wamepigwa marufuku kuvuka mto kipindi wanapokuwa kwenye hedhi.

Kwa mujibu wa utafiti huo, hali ya watoto imeimarika katika nchi 95 kati ya 175 duniani zilizofanyiwa utafiti lakini hali ilionekana kushuka katika mataifa 40.

Nchi iliopo chini ya orodha hiyo ni Niger pamoja na Mali na Jamhuri ya Afrika ya kati - huku matiafa 8 kati ya kumi ya mwisho kutoka Afrika magharibi au ya kati.

Save the Children limetaja kwamba licha ya kukithiri kwa uchumi na nguvu za kijeshi, Marekani katika nafasi ya (36) Urusi (37) na China (40) zote zimo nyuma ya mataifa ya Ulaya magharibi.

Huenda ukavutia na hii pia:

Shirika la save the children limetaja mambo kadhaa linalosema yanahitaji kushughulikiwa kwa hatua za pamoja.

  • Kuongezeka kwa mimba za utotoni.
  • Idadi ya ndoa za wasichana walio na umri wa chini ya miaka 18.
  • Pengo linaloongezeka kati ya nchi tajiri na maskini.
  • Hali inayozidi kuwa mbaya kuishi kusini mwa jangwa la Sahara.
  • Utumikishwaji wa watoto.
  • Jitihada zilizokwama kushinikiza elimu kote duniani.
  • Idadi kubwa ya watu waliochwa bila ya makaazi duniani.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Watoto duniani wanakabiliwa na umaskini,mizozo, na kunyimwa kukuwa kama watoto kwa kuishiwa kutumikishwa

Shirika hilo limesema watu 20 wanaachwa bila ya makaazi kila dakika kutokana na mizozo au unyanyasaji.

Shirika hilo limekabiliwa na uchunguzi kwa tuhuma za unyanyasaji wa kingono wakati kukiwa na kashfa kubwa zaidi ya wafanyakazi wa mashirika ya misaada ya mataifa ya magharibi.