Je Israel inachochea uhasama kati ya Urusi na Iran?

Vifaru vya Israeli katika maeneo ya Golan Heights (May 2018)

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Israel imeimarisha ulinzi wake katika maeneo ya Golan ambayo yako mpakani na Syria

Mapema mwezi huu mgogoro wa muda mrefu kati ya Israel na Iran nchini Syria uliongezeka. kile kinachoaminika kuwa shambulio la roketi la Iran dhidi ya maeneo ya jeshi la Israel katika milima ya Golan{ ikiwa ni hatua ya kulipiza kisasi mashambulio ya Israel dhidi ya kambi za kijeshi za Iran nchini humo yalisababaisha majibu makali ya kijeshi kutoka Israel.

Ndege za kijeshi za Israel zilishambulia maeneo 50 ya Iran nchini Syria hususan kila kambi ya kijeshi ya Iran ama vituo vyake kulingana na wachanganuzi, swala lililolemaza kasi ya Iran kuimarisha uwepo wake kwa miezi kadhaa iwapo sio miaka.

Lakini sasa inaendelea kuwa wazi kwamba shambulio hilo linaweza kubadili mienendo ya kikanda zaidi.

Na yaliojiri kutoka maeneo ya kusini ya milima ya Golan yanaweza kuongeza msukumo zaidi.

Eneo hilo lililopo kusini magharibi mwa Syria linaloshirikisha jimbo la Quneitra ambalo liko mpakani na Israel linaonekana kuangaziwa na serikali hiyo.

Serikali ya Assad iko tayari kuvifurusha vikosi kadhaa vya kijeshi, baadhi yao vikitii kundi la Islamic State. Mgogoro mpya unaweza kuzua wasiwasi miongoni mwa mataifa hayo matatu yalio na maslahi makubwa nchin Syria -Iran, Israel na Urusi.

Kupima mambo

Uhusiano kati ya mataifa hayo matatu sio wa kawaida . Iran na Israel ni maadui wakubwa. Na taifa la Syria linaelekea kuwa eneo hatari zaidi katika uadui wao.

Urusi na Iran zimekuwa zikiisaidia serikali ya rais Assad nchini Syria ,bila usaidizi wao pengine kufikia sasa angekuwa ameng'olewa madarakani.

Lakini Urusi pia ina uhusiano wa karibu na Israel. Waziri mkuu wa Israel Bejamini Netanyahu hivi majuzi alikuwa mgeni katika gwaride la kijeshi mjini Moscow kuadhimisha ushindi wao katika vita vya pili vya dunia.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Russia haijaingilia kati wakati Israel ilipoishambulia Syria

Je Urusi inapima vipi uzani wake wa uhusiano na Iran pamoja na Israel? Je inalinda maslahi yake kutoka nchi zote tatu nchini Syria?

Swala la kushangaza katika kampeni ya mashambulizi ya Israel ya kuzuia ama hata kupunguza kasi ya majeshi ya Iran kujiimarisha nchini Syria ni swala ambalo Moscow imekataa kuangazia.

Urusi ambayo ni rafiki wa Iran ina kambi zake za kijeshi nchini Syria ikiwa na rada ya kiwango cha juu mbali na makombora yanayoweza kudhoofisha operesheni za angani za Israel iwapo inataka kufanya hivyo.

Lakini kufikia sasa haijachukua hatua yoyote.

Badala yake limeiwacha anga ya Syria na Lebanon wazi kwa operesheni za angani za Israel kuendelezwa. Ni kweli kwamba kuna mpaka kati ya Israel na makao makuu ya Urusi nchini Syria ili kuhakikisha kuwa mashambulio ya Israel hayahitilafiani na mienendo ya anagni ya Urusi.

Maslahi

Ni hitimisho gani ambalo linafaa kufananishwa na tabia za Urusi?

Je kuna uwezekano kwamba Urusi na Iran zimevunja uhusiano wao wa karibu?

Na je uamuzi huo unamaanisha nini kuhusu vita ambavyo havijatangazwa kati ya Israel na Iran?

Mwanzoni ilikuwa rahisi. Wakati serikali ya Assad ilipoonekana kuanguka 2016, washirika wake walilazimika kumsaidia.

Urusi ilitoa usaidizi wa angani na ilikuwa Iran na wanamgambo wake wakiwemo Hezbollah nchini Lebanon waliopiga jeki vikosi vya rais Assad ardhini.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Chini ya usimamizi wa Qassem Soleimani (katikati), Iran imeimarisha uwez wa majeshi yake nchini Syria

Katika hali hiyo, Urusi na Iran zilikuwa na malengo ya kurudisha udhabiti wa hali ya kijeshi na kuisaidia serikali ya Syria kutekeleza mashambulizi kwa lengo la kukomboa maeneo yake yaliokuwa yametekwa.

Kwa pande wa Urusi hatua hiyo ililenga kumsaidia mwandani wake wa muda mrefu tangu zama za miaka ya vita baridi.

Urusi ilishangazwa na ukosefu wa udhabiti katika eneo hilo ikihofia kwamba ushawishi wa Islamic state huenda ukaingia hadi karibu na mpaka wake.