Programu ya AfyaDATA yatoa matumaini katika vita dhidi ya Ebola DRC
Huwezi kusikiliza tena

Teknolojia ya Kitanzania kusaidia vita dhidi ya Ebola DRC

Huku matukio ya vifo vitokanavyo na ugonjwa wa Ebola yakiripotiwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, serikali ya nchi hiyo imewasilisha ombi kwa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine Tanzania (SUA) ili waweze kutumia nyenzo ya AfyaDATA sambamba na wataalam wake kwa ajili ya kupambana na ugonjwa huo.

Nyenzo hiyo ambayo inaweza kugundua iwapo mtu ama mnyama anakimelea cha ugonjwa, inaweza pia kutuma taarifa kwa haraka na kusaidia kuzuia magonjwa hususan ya milipuko.

Mada zinazohusiana