Uraibu wa Tramadol wachochea machafuko Nigeria

Mji wa Maiduguri umegubikwa na machafuko katika vita dhidi ya Boko Haram - lakini pia unapambana kimya kimya na vita dhidi ya madawa
Image caption Mji wa Maiduguri umegubikwa na machafuko katika vita dhidi ya Boko Haram - lakini pia unapambana kimya kimya na vita dhidi ya madawa

Baada ya uchunguzi wa BBC mwezi Aprili kuonyesha uraibu wa dawa aina ya codeine nchini Nigeria, uzalishaji wa dawa hiyo ya maji ulipigwa marufuku Nigeria.

Lakini si codeine pekee iliyosambaa Afrika Magharibi, dawa nyingine ya kuponya maumivu, Tramadol pia inaelezwa kuwa hutumika kama kilevi. Mwandishi wa BBC, Stephanie Hegarty amebaini kuwa uraibu huo huenda ukachochea uasi Kaskazini Mashariki.

Wakati Mustafa Kolo, mwenye miaka 23 akimeza dawa nyekundu huhisi kama vile anaweza kusukuma mti, ni kama vile mwili si wake.

''Ninapomeza, nasahau kila kitu,'' anaeleza.

Macho ya Kolo ni mekundu, anaongea kama mtu aliyelewa,kichwa chake kikinesanesa.

''Nilizoea kumeza vidonge vitatu mpaka vinne nilipoanza kutumia. Lakini sasa nimepunguza mpaka kidonge kimoja au nusu''.

Image caption Mustafa Kolo asema dawa hizo humsaidia anapokuwa msituni akipigana na Boko Haram

Katika mji wa Maiduguri, maelfu ya watu wamezama kwenye uraibu wa dawa ya Tramadol.

Dawa hii ya kupambana na maumivu ambayo gharama yake ni ya chini hutibu maumivu,lakini nyingi zina uraibu,suala la ni kwa namna gani bado linajadilika.

Uraibu wa Tramadol

''Tatizo hili ni kubwa sana,anasema Marcus Ayuba,mkuu wa shirika la utekelezaji wa sheria ya madawa katika jimbo la Borno.

Ayuba anasema mtu mmoja kati ya watatu wana uraibu wa dawa hizo.

''Watu wamepoteza kila kitu,anasema.''kuna vijana ambao walikuwa wakulima, wamepoteza mashamba yao na makazi yao''.

Image caption Tramadol inaingia Nigeria ikiwa imefichwa katika dawa nyengine BBC imegundua

''Wazazi wameshuudia watoto wao wakiuawa mbele yao''.Ameongeza.

Lakini machafuko hayakuileta Tramadol Nigeria.Bwana Kolo alianza kutumia Tramadol mwaka 2007,miaka miwili kabla ya kuanza uasi.

Kwanza anasema ilikuwa ikimsaidia kazini.ilikua ikimuondolea maumivu na kumsaidia kutozidiwa na usingizi.

lakini sasa kutokana na uraibu,hawezi kupata kazi badala yake anajitolea kufanya kazi kwenye jamii.

''Inanisaidia kupambana na Boko Haram'' ninapokuwa porini,hata namna ninavyokimbia, ninavyotembea,ni tofauti.Inanipa nguvu''.

Tramadol ni nini

  • Dawa ya kutibu maumivu
  • Inatibu msongo na matatizo ya wanaume kufika kileleni mapema wakati wa kujamiiana
  • Tramadol hupatikana kisheria kwa maelekezo ya Daktari nchini Nigeria
  • lakini inapatikana kwa wingi kwenye maduka ya dawa nchi nzima
  • Dawa ya Tramadol huingia kwa wingi nchini Nigeria kutokea India

Tramadol ilikuwa ikitumika kwa viongozi na wanaokwenda kwenye mapigano.Inaaminika kuwa wapiganaji wa zamani wote walikuwa wana uraibu.

Bwana Ayuba anasema namna watu walivyokuwa wakitumia dawa hizo kisha wakatumwa kwenda kuua inaogopesha na anaamini kuwa dawa hizo zimechangia vitendo vya ukatili katika mzozo huu.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii