Mgogoro wa bahari ya kusini mwa China: Marekani yasema China 'inawatishia majirani zake'

Bejing imekuwa ikivibadilisha visiwa hivyo kuwa kambi zake za kijeshi Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Bejing imekuwa ikivibadilisha visiwa hivyo kuwa kambi zake za kijeshi

China inapeleka silaha katika eneo la bahari ya kusini mwa nchi hiyo ili kuwatishia na kuwashurutisha majirani zake, waziri wa Ulinzi wa Marekani James Mattis amesema.

Akizungumza nchini Singapore, Jenerali Mattis alisema kuwa vitendo vya Beijing vinazua maswali mengi kuhusu malengo yake.

Pia alisema kuwa swala la vikosi vya kijeshi vya marekani nchini Korea Kusini halitazungumziwa katika mkutano wa mwezi huu kati ya rais Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un.

Marekani imetaka mataifa ya rasi ya Korea kusitisha kabisa mipango ya kinyuklia, aliongezea.

Waziri wa Uinzi nchini Korea Kusini Song Young-moo pia aliambia mkutano wa usalama wa Shangri-La Dialogue kwamba majeshi ya Marekani nchini Korea Kusini ni swala tofauti na lile la mpango wa kinyuklia wa Korea Kaskazini.

Kuna takriban wanajeshi 28,500 wa Marekani Korea Kusini.

Bwana Mattis aliambia mkutano huo wa usalama kwamba Beijing ilipeleka silaha ikiwemo zile za kushambulia meli ,makombora ya kudungua ndege katika maeneo yaliopo katika bahari ya kusini mwa China.

''Licha ya madai ya China kukana, silaha hizo zimewekwa tayari kwa matumizi ya moja kwa moja ya kijeshi kwa lengo la kutishia na kuwashurutisha majirani zake'' , alisema Jenerali Mattis.

Jenerali Mattis alisema kuwa utawala wa rais Trump ulitaka uhusiano mzuri na China lakini utashindana na taifa hilo kwa hali na mali iwapo utahitajika kufanya hivyo.

Image caption Ramani ya Visiwa vya bahari ya kusini mwa China

Alisema kuwa Marekani inatambua kwamba China ina jukumu katika eneo hilo. Bahari hiyo ya Kusini mwa Korea ambayo ni njia muhimu ya kibiashara inagombaniwa na mataifa sita.

China imekuwa ikijenga visiwa vidogo na vipengee vyengine katika eneo hilo.

Mwezi uliopita China ilisema kuwa kwa mara ya kwanza iliwasilisha makombora katika kisiwa cha Woody na kisiwa cha Paracel na hivyobasi kupata onyo kutoka kwa Marekani kwamba inaleta wasiwasi wa kiusalama katika eneo hilo

Kisiwa cha woody, kinachoitwa Yongxing na China pia kinapiganiwa na Vietnam pamoja na Taiwan.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii