Ujumbe wa simu unavyoweza kuokoa maisha ya wavuvi

Mara nyingi shughuli za uvuvi hufanyika usiku muda ambao vimbunga huweza kutokea kirahisi Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mara nyingi shughuli za uvuvi hufanyika usiku muda ambao vimbunga huweza kutokea kirahisi

Hatuwezi kuzuia uhalisia unapoachilia ghadhabu yake kwa mtindo wa Volkano, tetemeko la ardhi , vimbunga na maporomoko ya theluji, Lakini teknolojia inaweza ikatupa ilani kuhusu hatari iliyo mbele yetu na kuokoa.

Jua linapozama Ziwa Victoria, kubwa kabisa barani Afrika,maelfu ya wavuvi huwa tayari kuelekea majini wakati wa usiku kwa ajili ya kuvua samaki hasa Sato na Sangara.

Wanapoingia majini, wanajua wanahatarisha maisha yao, baadhi yao huenda wasionekane tena.

Ziwa Victoria linatumiwa na Uganda, Tanzania na Kenya, hukumbwa na vimbunga hatari, mwaka huu, upepo mkali, mvua, radi na mawimbi makubwa vinajitokeza.

Mabadiliko ya tabia nchi yatishia wavuvi Ziwa Victoria

Wavuvi mpaka 5,000 hupoteza maisha kila mwaka, Shirika la kimataifa la msalaba mwekundu limeeleza.

''Vimbunga mara nyingi huanza usiku wa manane mpaka saa kumi na mbili asubuhi'', anaeleza Amone Pansiano, afisa wa askariwa majini katika kisiwa cha Nkose, Uganda.

''Muda huu ndio haswa muda ambao wavuvi wako na kazi nyingi, wakikusanya nyavu.Ni hatari na watu wengi wametoweka.''

Haki miliki ya picha Amone Ponsiano
Image caption Askari wa majini Amone Ponsiano anasema wavuvi wengi hutoweka wakati wa kimbunga

Hivi karibuni, Boti ya mtu mmoja iligonga miamba alipokuwa akikwepa dhoruba ya kimbunga, lakini kikosi cha Ponsiano kiliweza kumuokoa

Lakini mfumo wa utoaji taarifa wa timu ya kimataifa ya wanasayansi ungeweza kuokoa maisha ya mamia

Data ya Satelaiti kutoka shirika la anga NASA huhusika katika kutabiri uwezekano wa kutokea kimbunga.Uwezekano huu huja kwa njia rahisi ya ujumbe wa tahadhari kwenda kwa wavuvi kupitia ujumbe mfupi wa simu, Twitter au WhatsApp.

Profesa Wim Thiery, kiongozi wa jopo la utafiti kuhusu mradi huu unaofanywa kwa ushirikiano kati ya Chuo cha Vrije Brussel kilicho Brussels, chuo cha ETH Zurich,Nasa na CodeForAfrica anasema kuna umuhimu wa kuwa na mfumo huu ili kuimarisha utabiri wa hali ya hewa.

Haki miliki ya picha TOMAZ KUNST/SHUTTERSTOCK
Image caption Vimbunga kwenye Ziwa Victoria vinaweza kuwa hatari na vyenye kuleta madhara makubwa

Mwaka 2014 Mwanafunzi wa fani ya uhandisi, Ahmad Wani alijikuta amakwama kwa juma moja akisubiri kuokolewa kutoka kwenye mafuriko katika jimbo la Kashmir India.Mafuriko yalisababisha mamia ya watu kupoteza maisha.

Tangu kutokea kwa tukio hilo ameweka akili yake kwenye kujipatia ujuzi katika kutengeneza mashine inayoweza kutabiri athari za majanga ya asili.Utabiri mzuri utawezesha jamii za mijini kujiandaa vyema,anaamini.

Wani anasema ''ifikapo mwaka 2030 asilimia 60 ya watu watakuwa wakiishi mjini.''

''Habari njema nni kuwa madhara yake yanaweza kubadilishwa.Kwa kuwa na ufahamu kuhusu kujiandaa, kukabili, kujinasua na hatari na kupunguza madhara ya majanga,viongozi wanaweza kupunguza madhara ambayo yanawakabili watu wao'',Alieleza Bwana Wani.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Barabara hii ya nchini Tajikistan ilipigwa na maporomoko ya theluji 40 Januari mwaka 2017 na kusababisha vifo vya watu wanane.

Takribani watu 150 wanapoteza maisha kutokana na maporomoko ya theluji.Lakini theluthi mbili ya watu wanaotumia simu za kiganjani, nusu yao aina ya smartphone, Maabara inayoshughulikia taarifa za majanga ya maporomoko ya theluji inaweza kuthibitisha kuwa application ya simu inaweza kuzuia majanga hayo, pia ni kifaa muhimu cha kusaidia uokoaji wakati wa majira ya baridi.

Inafanya watu walio nje kwenye mazingira yenye barafu kuweza kuchunguza barafu na kutuma ujumbe kwenye ramani ya Data kusambaza ujumbe kwa jamii, pia utabiri wa hali ya hewa unaweza kutolewa kwa kutumia app hiyo ili kusaidia watumiaji kufanya maamuzi sahihi kabla ya kutoka.