Trump sasa anatarajiwa kukutana na Kiongozi wa Korea kaskazini kisiwani Sentosa Singapore

Kim Jong-un atakutana na Donald Trump kisiwani Sentosa, Singapore Haki miliki ya picha EPA
Image caption Kim Jong-un atakutana na Donald Trump kisiwani Sentosa, Singapore Juni 12

Mkutano unaosubiriwa kwa hamu kati ya rais wa Marekani Donald Trump na kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong-un utafanyika katika hoteli moja kwenye kisiwa cha Sentosa, Singapore, ikulu ya Marekani imethibitisha.

Mkutano huo wa kihistoria utafanyika Juni 12, lakini taarifa nyingi bado haizjathibitishwa.

Itakuwa mkutano wa kwanza kati ya kiongozi wa Korea kaskazini na rais aliyepo madarakani wa Marekani.

Siku ya Jumanne usiku Trump amesema 'mipango inaendelea vizuri'.

"Uhusiano mwingi unaundwa, majadiliano makubwa yanaendelea kabla ya safari," amewaambia waandishi.

Lakini inavyoonekana ni kwamba watakaa katika hoteli tofauti Singapore, kwa mujiu wa ripoti katika gazeti la Straits Times . Hoteli hizo mbili zipo katika kisiwa kikuu .

Sentosa ni mojawapo ya visiwa 63 vya Singapore.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Je tunashuhudia sura mpya ya Kim Jong-un katika siasa?

Kim Jong-un: Kiongozi mpya mwenye umaarufu katika siasa za Dunia

Ghafla Kim Jong-un amekuwa kiongozi mpya mwenye umaarufu katika siasa za 2018.

Baada ya kuwa kando kwa miaka mingi, ameibuka kuwa kiongozi mwenye nguvu.

Viongozi kutoka China, Urusi, Syria Korea kusini na Marekani wote wamekutana au awanatarajiwa kukutana na Bwana Kim mwaka huu.

Haki miliki ya picha Getty/Composite
Image caption Rais Assad (kushoto) na Putin (kulia) wameelezea matumaini ya kukutana na bwana Kim (kati)

Wanafuatana kwa msururu. Vladimir Putin amemualika aende Vladivostock Septemba na rais wa Syria Assad amesema pia angependa kuitembelea Pyongyang.

"Huu ni mwanzo mpya wa kimataifa ulio tofuati kabisa kuliko tulivyoshuhudia mnamo 2010, wakati Kim Jong Un alipojitokeza kama mtu asiyejulikana, kijana aliyetazamiwa kuwa mrithi wa uongozi.

"Sasa akiwa amejihami kwa silaha nzito, Kim anajitokeza kama kiongozi wa nchi inayojitazama kama nchi yenye nguvu za nyuklia sambamba na nchi nyingine duniani zenye silaha za nyuklia ikiwemo Marekani. " anasema Jean Lee, aliyekuwa mhariri mkuu wa shirika la habari la Associated Press Pyongyang.

Baada ya Kim Jong-un.kutangaza kuwa mapngo wake wa silaha umekamilika, alitangaza kuwa lengo lake kuu ni kushughulikia uchumi.

Na ili kuweza kufanya hivyo alihitaji kuunda uhusiano na kufufua urafiki wa zamani.

Kituo cha kwanza kilikuwa China, mshirika mkuu wa kibiashara wa Korea kaskazini.

Rasi Xi Jinping alisaidia kuidhinisha shinikizo kamili la Donald Trump mwishoni mwa 2017, na kukatiza bidhaa muhimu hatua ambayo iliipa Pyongyang kichefu chefu.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kim na rais Xi walipigwa picha wakati wa mkutano huo

Lakini sasa Kim safari haziishi. Ameizuru China mara mbili chini ya miezi miwili.

Ilikuwa na hisia zilizoibuka katika mkutano wa kihistoria mnamo Aprili katika mpaka wa Korea na kiongozi wa Korea kusini Moon Jae-in.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Bwana Moon na Kim walikumbatiana wakati ulimwengu ukitazama

Alichukua hatua nyingine kama hiyo na Moscow wiki iliyopita. Aliyekuwa mkuu wa ujasusi wa Korea kaskazini Kim Yong-chol alipokuwa njiani kwenda Marekani, Kim aliamua sasa kumkaribisha Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov mjini Pyongyang.

Korea Kusini yaiwekea vikwazo Korea Kaskazini

Ilikuwa ni ziara ya kwanza ya mwanadiplomasi amkuu wa Urusi katika muda unaozidi mwongo mmoja.

Huenda ni sadfa, lakini ni jambo ambalo halikumfurahisha Donald Trump.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ziara ya waziri wa Urusi Lavrov Pyongyang

So iwapo Washington ilidhani kwamba Korea kaskazini imekwama , Kim Jong-un anatuma ujumbe na kudhihirisha hadharani nafasi nyingine alizo nazo.

Amebadili sheria za mchezo. Mwaka jana alijigamba kwa uwezo wake wa nyuklia, sasa anazitumia kama silaha ya kidiplomasia.

Lakini suali kuu ni je Mchezo huu wa Korea kaskazini utakwishaje? Na ni kitu gani kitakachofanyika baada ya mkutano?

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii