Rais Museveni ataka marufuku ya plastiki itekelezwe Uganda

Sababu kuu ya kuidhinisha marufuku hiyo plastiki ni kusaidia kulinda mazingira.
Maelezo ya picha,

Sababu kuu ya kuidhinisha marufuku hiyo plastiki ni kusaidia kulinda mazingira.

Rais Yoweri Museveni ameamrisha maafisa wa usalama nchini kuhakikisha kuwa marufuku ya kutumia mifuko ya plastiki nchini inatekelezwa.

Ametaka kampuni 45 nchini za kutengeneza plastiki kusitisha utengenezaji wa mifuko ya plastiki katika hatua ya kufufua marufuku ya serikali ambayo imekuwepo lakini isiyotekelezwa.

"Marufuku ya utengenezaji, usambazaji na uuzaji na matumizi haijafutiliwa mbali na inapswa kutekelezwa, alisema Museveni.

Sheria ya mwaka 2009 ya fedha inapiga marufuku "uingizaji, utengenezaji, uuzaji na utumiaji wa mifuko na magunia ya plastiki kuanzia Machi 31, mwaka 2010.

Hatahivyo kama ilivyo kwa baadhi ya mataifa yalioendelea, utekelezaji wa sheria hiyo ndio tatizo, ni nchini Uganda ni kama ambaye ziligonga mwamba kufuatia tofuati zilizoibuka miongoni mwa mawaziri nchini huku kukiwepo shinikizo kutoka kwa watengenezaji wa plastiki.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Museveni ameamrisha maafisa wa usalama nchini kuhakikisha kuwa marufuku ya kutumia mifuko ya plastiki nchini inatekelezwa

Makampuni ya kutenegenza mifuko hiyo yamelalamika kuwa kuidhinishwa kwa marufuku bila ya kuwepo kwa matumizi mbadala kunawaweka katika hali mbaa wauzaji wa bidhaa madukani kwa kutokuwana mahali pa kuwawekea wateja vbidhaa hizo.

Na pia kwamba itafunga nafasi za ajirawakati viwanda vinapunguza utengenezaji wa mifuko hiyo.

Uganda ni miongoni mwa nchi za Afrika zilizoidhinisha marufuku ya kutumia , kuuza au kutengeneza mifuko ya plastiki.

Kenya imepiga marufuku mifuko hiyo mnamo 2017 na imeorodheshwa miongoni mwa mataifa 50 yaliochukuwa hatua hiyo katika ripoti kubwa ya Umoja wa mataifa kuwahi kutolewa inayopendekeza kuwa serikali duniani zinahitaji kufikiria kupiga marufuku au kuidhinisha kodi kubwa kwa watengenezaji mifuko hiyo ya plastiki.

Katika baadhi ya mataifa , kuna sheria dhidi ya matumizi ya plastiki lakini tatizo linakuwa katika utekelezaji wa sheria hizo.

Hali ilivyo kwa mataifa:

  • Botswana - wauzaji hulipishwa lakini hakuna utekelezaji wa sheria.
  • Eritrea - Mifuko ya plastiki imepigwa marufuku na kumepunguwa mafuriko ya mirtaro na mashimo ya maji taka
  • Gambia - Mifuko imepigwa marufuku lakini imezuka upya baada ya mzozo wa kisiasa.
  • Morocco - Mifuko imepigwa marufuku - tani 421 zilinaswa kwa mwaka mmoja, na watu wanatumia mifuko ya vitambara badala yake.
  • Bangladesh - Marufuku imeidhinishwa na utekelezaji wa sheria ni tatizo
  • China - ilikuwa ikitumia mifuko bilini 3 kwa mwaka, sasa imeidhinishwa marufuku ya mifuko mepesi.
  • Vietnam - bags are taxed but still widely used. Government considering increasing tax five times
  • Ireland - kodi kubwa inayotozwa imechangia kupungua kwa matumizi kwa 90%
  • Kenya - mifugo hula takriban mifuko 2 na nusu maishani mwao. sasa marufuku imeidhinishwa na adhabu kali hutolewa kwa kuunda, kuingiza au kutumia mifuko ya plastiki.

Mifuko ya plastiki hukwama katika mitaro na mashimo ya maji taka na kusababisha mafuriko mvua inaponyesha na mara nyengine mifugo huyala mifuko hiyo wanapokuwa malishoni.

Ripoti hiyo ya Umoja wamataifa inasema kumeshuhudiwa matokeo tofuati katika sera za kupambana na taka za palstiki. Nchini Cameroon, mifuko ya plastiki imepigwa marufuku na watu majumbani hulipwa kwa kila kilo ya taka za plastiki wanazokusanya, lakini bado mifuko hiyo huingizwa kwa njia za kimagendo nchini.