Mawasiliano ya pembeni na watu wa jinsia tofauti mtandaoni yanafaa?

Matumizi mabaya ya teknolojia ya simu husababisha usaliti baina ya wapenzi

Chanzo cha picha, Danae Diaz

Maelezo ya picha,

Matumizi mabaya ya teknolojia ya simu husababisha usaliti baina ya wapenzi

Hapo zamani, kuchepuka (kuwa na mpango wa kando) kulikuwa kunagundulika kwa kutazama rangi ya mdomo kwenye kola ya shati, harufu ya manukato au risiti kwenye mfuko wa suruali.

Mtu aliweza kugundua kama mwenza amekuwa akifanya vitu ambavyo hatakiwi kuvifanya, lakini katika huu ulimwengu wa kuwa na App za wapenzi kukutana na ujumbe wa maneno kwa faragha, mambo yamekuwa magumu zaidi.

Kuna sasa msamiati mpya micro-cheating: Jina hili linaeleza kuwa vitu vidogo ambavyo unaweza kufikiri kuwa sio vibaya, lakini vinaweza kuwa vibaya, hapo ndipo panapokufanya kuwa njia panda-ni nini maana ya kuchepuka kidogo (micro-cheating) na je kuna kitu kama '' kuchepuka kidogo tu''?

Ndio, anasema Dokta Martin Graff, Profesa wa Saikolojia katika Chuo kikuu cha South Wales, ambaye ni mtaalamu.

Aliandika kuhusu masuala ya kuwa na mahusiano ya katika ulimwengu wa kisasa, katika makala yake kwenye jarida la saikolojia hivi karibuni alieleza kuhusu namna ambavyo kukosa uaminifu unavyokua tunavyoendelea kuishi katika maisha ya mitandao.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Usaliti ni nini ?

Dokta Graff anatafsiri neno hili la micro- cheating kuwa kitendo au tabia inayofanywa na mtu ambaye yuko kwenye mahusiano ambaye anakuwa akionyesha kwa mtu mwingine wa tatu kuwa anaweza kupatikana kihisia kwa mtu huyo.

Kabla ya Smartphone, uchepukaji huu mdogomdogo (micro-cheating) kulikuwa ni kama vile kuvua pete ya ndoa kisirisiri unapotoka nje, lakini katika ulimwengu wa dijitali ni rahisi zaidi kumpa ishara mtu kuwa unaweza kupatikana kimapenzi, kwa mfano kutembelea picha za zamani za kwanza kabisa za mtu katika ukurasa wa Instagram na kutuma ujumbe wa moja kwa moja kwake.

Nichi Hodgson, ambaye ameandika kitabu kuelezea historia ya mahusiano, anakubali kuwa (micro-cheating) ni jina la tabia za zamani.

''Hata katika karne ya 18, watu walikuwa wakipeana ishara za kutakana kimapenzi kwa kutumia barua, lakini sasa kilichobadilika ni kuwa sasa tunatumia vifaa ambavyo kutekeleza azma hiyo ni rahisi mno kuliko hapo awali.

Hata hivyo, kama alivyoainisha Dokta Graff, wakati micro-cheating inaweza isiwe kumsaliti mwenza,ni tabia ambayo inaweza kuchochea hali ya kukosa uaminifu.

''Ukweli ni kwamba tunawasiliana zaidi kwa njia ya mitandaoni kuliko ana kwa ana, hali hii inafanya mahusiano kutoeleweka

Graff,Nichi na mtaalamu wa masuala ya mahusiano, Leila Collins wanaeleza namna ambayo utajua kuwa unasalitiwa au kusaliti.

Chanzo cha picha, Danae Diaz

Maelezo ya picha,

Vitu ambavyo huonekana kama vidogo vidogo huonekana vikubwa kwenye mahusiano

Kumtumia ujumbe mpenzi wa zamani

Uko na mweza wako lakini mara una shauku ya kuwasiliana na mpenzi wako wa zamani unapiga picha kisha unamtumia: kisha anajibu na kuweka alama ya busu mwishoni mwa ujumbe wake.Ikiwa utaendelea na majibizano hayo ya kwenye simu , unafanya usaliti?.

Mtaalamu anasema:

Nichi: Si jambo baya kuwa na mawasiliano na mpenzi wa zamani, hasa kama hamuwasiliani kwa siri kwa ajili ya mapatano au katika kutaka kumfanya mpenzi wa zamani akutamani tena,watu wengi wanawatumia ujumbe wapenzi wa zamani hasa wakijua kuwa wapenzi wao wa zamani bado wana hisia nao za kimapenzi.''

Leila: "Kwa nini utake kuwa na mawasiliano na mpenzi wako wa zamani kama mlikubaliana kuwa mahusiano baina yenu yamefika mwisho? haijalishi nia ni nini hasa, ni dalili mbaya, nitaiweka kwenye kundi la usaliti''.

Kupenda picha za mtu mwingine kwenye mtandao wa kijamii:

Uko kitandani.Umezima taa lakini huwezi kulala, kidole chako kinabonyezabonyeza simu na kuanza kupitia Instagram.Unanza kubonyeza alama ya kupenda picha ya mtu mwingine ambaye kama usingekuwa kwenye mahusiano angekuwa mwenza wako,kisha unafanya hivyohiyo wakati wa mapumziko ya chakula cha mchana na njiani ukiwa kwenye basi unaacha alama za emoji kwenye picha zao za hivi karibuni ikiwemo.

Wataalamu wanasemaje?

Nichi : ''Watu wengi hawalifurahii jambo hili, na pengine ni dalili kuwa kuna tatizo kubwa kwenye mahusiano yao.Kupenda posti za wengine mtandaoni si lazima liwe jambo la kukufanya ujisikie vibaya, lakini kama mara nyingi unapenda posti za mtu huyohuyo tu, linaweza kuwa tatizo.

Chanzo cha picha, Danae Diaz

Maelezo ya picha,

Hii inaonyesha kuwa mahusiano ya watu hawa yana tatizo kubwa

Kutengeneza urafiki usio wa kingono mtandaoni

Unakwenda mapumziko na wanafunzi wenzio wa Chuo na ukawa na ukaribu na mmoja wao .Mkawa marafiki wa Facebook mliporejea.Kuanzia hapo mkaendeleza urafiki mpaka Instagram.Mara ukiwa kwenye basi kuelekea nyumbani unapata ujumbe akikuomba namba yako ya simu ili mzungumze kuhusu masomo.

Leila:''lazima uwe mkweli na kuheshimu, kama uko kwenye mahusiano na unafanya mambo haya kama vile kujenga mahusiano na mtu mwingine au kuwatumia ujumbe watu wengine, ni makosa.''

Nichi: ''Ni wazi huwa tunakutana na watu ambao tuna maono yanayofanana, sifikirii kama kuna ubaya, lakini lazima uwe wazi kuhusu uhusiano wenu kwa kuwa mtu mwingine anaweza kutafsiri vibaya urafiki .Ikiwa utaanza kupokea ujumbe kwa siri na kuwa na mawasiliano ya siri, basi itakuwa kuna jambo limefichwa.

Kutojiondoa kwenye App za mahusiano

Sote tumepita huko.Baada ya miezi ya kuwa kwenye app za mahusiano, sasa ni miezi kadhaa na uko kwenye uhusiano wa kweli.

Ni vizuri, lakini huwezi kufuta app hiyo na mara nyingine unajikuta mara kadhaa unaingia mitandaoni kama ukiwa mpweke.

Wataalamu wasema

Nichi: "kutojiondoa kwenye mtandao si sawa.Inamfanya mtu mwingine kuwa na shauku kwa kuwa hujamfuta.''

Leila: ''Hii haikubaliki, kwa nini ukawa na mahusiano na mtu mwingine huku ukiwa kwenye mahusiano? Ninaona mawasiliano yote ambayo huwezi kuyaweka wazi kwa mwenza wako ni usaliti, si vinginevyo.