Ubaguzi wa rangi: Je wasanii weusi wenye rangi 'nyeupe' hufanikiwa rahisi katika sekta ya burudani?

Beyonce and Rihanna Haki miliki ya picha Getty Images

Rihanna, Beyonce, Cardi B, Stefflon Don, Maya Jama, Mabel, Zendaya na Adwoa Aboah.

Hawa ni miongoni mwa baadhi ya wanawake waliofanikiwa katika fani ya burudani 2018.

Lakini je ni kiwango gani cha ufanisi wao kinachotokana na rangi ya ngozi yao. Imedaiwa kwamba wanawake weusi wenye ngozi nyeupe hubahatika kujiendeleza kutokana na rangi yao.

Ubaguzi wa rangi huwachukiza watu wenye rangi nyeusi ama watu weusi wenye rangi nyeupe. Ni kitu ambacho msanii Lioness anasema amepata uzoefu wake.

Haki miliki ya picha @sjp_p @kevstakespics
Image caption Lioness anaesma kuwa aliwacha kufanya kitu alichokua akipenda kutokana na ubaguzi wa rangi.

Aliambia Newsbeat kwamba alijizulu katika fani ya muziki kwa miaka 7 na sababu kuu ilikuwa ubaguzi dhidi ya rangi yake nyeusi.

Wasakaji talanta wa A& B wangesema vitu kama hivi: Angekuwa bora iwapo angekuwa na rangi nyeupe -''mshororo huo kwangu hauna maana yoyote. najua kile wanachojaribu kusema, kwamba iwapo ningekuwa na ngozi ya rangi nyeupe ningefika mbali.

Kila unapoambiwa hilo na nikiwa kijana kama nilivyokuwa sikupendelea. Hivyobasi niliwacha kufanya kitu nilichokipenda kwa sababu watu walikuwa wakizungumzia kuhusu rangi yangu.

  • 'Upendeleo wa rangi nyeupe'

Swala la ubaguzi wa rangi lilizushwa tena hivi majuzi baada ya Maya Jama kuangazia swala hilo katika mzaha aliochapisha katika mtandao wa Twitter 2012 ambao uliwakasirisha wanawake wenye rangi nyeusi.

Baadhi ya watu katika mtandao wa kijamii walidai kwamba kazi ya mtangazaji huyo wa radio 1 ilipendelewa kutokana na rangi yake nyeupe.

Babake Beyonce Matthew Knowles pia alidai kwamba watu weusi wanapata umaarufu mkubwa kwa kuwa wana ngozi nyeupe mapema mwaka huu.

Alidai kwamba mwanawe alipata mafanikio makubwa kutokana na rangi yake ya ngozi akidai kwamba hakuna msanii mwenye ngozi ya rangi nyeusi aliyefanikiwa katika kipindi cha muongo mmoja uliopita.

Kati ya wanawake 68 ambao ni wanamuziki ambao wako katika orodha ya nyimbo 40 bora Uingereza tangu mwanzo wa 2017, 17 wana mizizi ya watu weusi huku wengi kati yao wakiwa na ngozi yenye rangi nyeupe.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption (L-R) Beyonce, Sza, Raye, Rihanna, Cardi B, Ella Eyre, Kelli-Leigh na Stefflon Don ote waliorodheshwa katika nyimbo 10 bora 2017

Kelli-Leigh, ambaye mamake ni mweusi na babake ni mweupe alikuwa katika orodha ya 10 bora katika wimbo wa James Hype, more than friends.

Alisema: "kwa sababu fulani nchini Uingereza , milango huwa imefungwa kwa wanamuziki wenye ngozi nyeusi- hatufai kukaguliwa kulingana na rangi zetu za ngozi tunafaa kuangiziwa kutokana na mitindo yetu.

Mwaka 2017 , Ray BLK alishinda taji la BBC Sound of Music lakini hajawahi kuwa na wimbo ulioorodheshwa katika nyimbo 40 bora ikilinganishwa na Jorja Smith na Raye, ambao pia walikuwa katika orodha hiyo.

Imezua maswali ya iwapo ngozi ya rangi yao ilichangia ufanisi wao.

Nicole Vassell, muhariri wa burudani pamoja na makala katika jarida la Pride magazine - llinalolenga wanawake weusi anasema: kuna sababu kwa nini idadi kubwa wa nyota wanaoenukia na nyota kadhaa katika fani ya burudani wana ngozi nyeupe.

Akina Beyonce ,Rihanna wanavipaji vizuri lakini rangi yao nyeupe imewapatia fursa kufika kule wanakotaka kufika.

Kunaweza kuwa na wanawake wenye rangu nyeusi ambao wana vipaji , lakini hatuwezi kuwajua kwa sababu hawapatiwi fursa.

Kila siku nilizidi kuwa mweusi zaidi ya nilivyokuwa hapo awali'

Mjadala kuhusu ubaguzi wa rangi umeenea hadi katika maeneo mengine ya sekta ya burudani.

Katika Filamu, waigizaji weusi wenye majukumu makubwa katika filamu 20 bora nchini Uingereza 2017 wanashirikisha Zoe Saldana, Tessa Thompson, Halle Berry, Elise Neal naNathalie Emmanuel.

Unapotazama majarida , majarida manne bora ya wanawake (Cosmopolitan, Vogue, Grazia na Marie Claire) yamekuwa na watu weusi tisa maarufu katika majarida 125 katika kurasa za mbele tangu Januari 2017.

Watu hao ni Rihanna, Meghan Markle, Beyonce, Adwoa Aboah, Lupita Nyong'o, Zoe Kravitz, Zoe Saldana, Jennifer Hudson na Gugu Mbatha-Raw.

Haki miliki ya picha PA

Megan Markle-binti mfalme wa Sussex alizungumzia kuhusu swala la ubaguzi wa rangi mwaka 2015 , akisema kuwa alipokuwa muigizaji alionekana kutokuwa na umuhimu wowote.

Akiandika katika jarida la Elle, alisema kuwa sababu kuu ya kuchukua jukumu la Rachel Zane katika kipindi cha kisheria nchini Marekani ni kwa sababu haikuwa sababu ya rangi yake

"Katika kipindi hicho watayarishaji hawakuwa wakimtafuta mtu mwenye rangi ama mtu mweupe ama mweusi .walikuwa wakimtafuta Rachel.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption (L-R) Zoe Kravitz, Zoe Saldana, Lupita Nyong'o, Adwoa Aboah, Gugu Mbatha-Raw and Jennifer Hudson have been on the front of top UK magazines since January 2017

Nyota wa filamu ya Sta wars Lupita Nyong'o amewahi kulalamika kuchekwa kwa rangi yake nyeusi na 'angemuomba mungu kuamka akiwa na rangi nyeupe'.

Muigizaji Adele Oni ambaye anaigiza kama mpiga picha katika filamu ya No Shade nchini Uingereza ambayo ni kuhusu ubaguzi wa rangi na mapenzi.

Haki miliki ya picha Tenisha White
Image caption Adele, ambaye anaigiza katika filamu ya Shade anasema kuwa ubaguzi wa rangi ni hadithi tusiyozungumza.

Anasema kuwa : Sote tunajua kwamba swala la rangi na lile la kukuwa na kuelewa kwamba iwapo wewe ni mweupe basi wewe ni mrembo mbele ya macho ya wanaume -na tunakubali.

'Kuna mabadiliko'

Vyombo vya habari na Burudani vimepongezwa kwa kuwaleta watu pamoja bila kuzingatia dini ama rangi.

Edward Enninful, muhariri wa kwanza mweusi wa jarida la Uingereza la Vogue alichukua kazi hiyo mnamo mwezi Agosti mwaka uliopita huku jarida la mwezi Mei likishirikisha wanawake waliokuwa na rangi tofauti

Na Black Panther, ambao waigizaji wake ni pamoja na Luipta Nyongo na Letitia Wright, ilipongezwa kwa kuwakilisha wanawake weusi katika filamu.

Jordan Mitchell, mkurugenzi mkuu wa kampuni ya mahusiano ya umma Liz Matthews PR, anasema kuwa mjadala kuhusu rangi mara nyengine huwashusha hadhi wanawake weusi

Haki miliki ya picha Alamy

Anasema kuwa kitu muhimu ni kupongeza hadhi ya burudani katika kuleta jamii tofauti pamoja . Najua kwamba mtu ambaye angewakilisha watu weusi angekuwa Halle Berry pekee.

Huku nikikidhania kwamba kwa sasa kuna wanawake wengi weusi walio na rangi tofauti nadhani kuna mabadiliko na mambo yameanza kuchukua mkondo mzuri.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii