Shakira hakuwa na matumaini ya kuimba tena baada ya kupoteza sauti

Shakira amerudi kwa kishindo baada ya kuugua Haki miliki ya picha XAVI MENOS
Image caption Shakira amerudi kwa kishindo baada ya kuugua

Baada ya kuahirisha ziara yake ya muziki ya El Dorado kwa miezi saba kutokana na tatizo la sauti, Hatimaye Shakira amerejea kwa kishindo juma lililopita akifanya tamasha moja kabambe

Ni ziara ya kwanza miaka saba baada ya kujipa muda wa kuanzisha familia na mumewe, mwanasoka wa Uhispania Gerard Pique.

Picha zilimuonesha mwanamuziki huyo mwenye miaka akiwa Hamburg akiwa mwenye furaha baada ya kurejea tena akiwa na afya njema

''Mwaka jana ulikuwa moja kati ya vipindi vigumu sana kwangu'', aliiambia BBC akiwa Amsterdam. ''Kurudi tena jukwaani imekuwa jambo la kunigusa mno''.

''Nilipata hisia kama vile ni mara ya kwanza,nyakati zilizopita nilikuwa naona tofauti kidogo, lakini sasa nikajisema ''ooh wamekuja kwa ajili yangu lazima nionekane vizuri na niimbe vizuri''.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Nyota wa Muziki akiwa na mumewe wakisheherekea ushindi wa Barcelona FC wa Copa del Rey mwaka 2015

Shakira amesema ni nafasi nyingine aliyoipata kuwafanya mashabiki watabasamu.

Shakira amesema alikuwa na shida ya sauti kiasi kwamba hakufikiri kama angeweza kurejea tena mbele ya hadhira na kuimba nyimbo zake.

Madaktari wake walifikiri kuwa angefanyiwa upasuaji lakini ilikuwa kama bahati tu alipona bila upasuaji, anasema ni kama miujiza

''Nakumbuka nilisali, nilisahau kusali muda , lakini ukipitia magumu mara unaanza kurejesha imani yako! nilimwambia Mungu kama nitatumia sauti yangu tena, nitashangilia kila siku-na ndicho nachofanya''.

Haki miliki ya picha SONY MUSIC
Image caption Shakira amekuwa mmoja kati ya watu wanaojitoa kwa ajili ya jamii

Mwaka jana, Jarida la Fortune lilimtaja Shakira kuwa miongoni wa viongozi 50 wa shughuli za kusaidia jamii.

amekuwa akijihusisha hasa kwenye sekta ya elimu, kazi aliyoanza kuifanya tangu alipokuwa na miaka 18, ambapo alianzisha mfuko wake kwa ajili ya kujenga shule katika maeneo duni nchini Colombia.

Shakira aliguswa kwa kuwa ametoka kwenye nchi zinazoendelea, alizaliwa na kukulia kwenye masikini jambo lililomuonyesha kuwa elimu ni msaada mkubwa katika kuyafikia mabadiliko.

Hivi sasa Shakira anayafurahia maisha yake ya kimuziki anasema ''Unapokuwa msanii unajisikia kwa kiasi fulani wanakutumia.Unawapa unachotaka.Lakini uhusiano huu umejengwa na mashabiki wangu kwa miaka mingi hivyo najisikia niko nao karibu zaidi, Inanifanya nijisikie wa thamani, ninayependwa na ndio maana nafurahia ukurasa wangu mpya wa maisha''.

Mada zinazohusiana