Kwa Picha: Kusalimiana kwa Donald Trump na Kim Jong Un na maana yake

Rais wa Marekani Donald Trump na Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un hatimaye wamesalimiana.

Lakini hakuna mtu alifahamu kile kingeendelea. Hapa tunachapisha picha kutoka mkutano huo kuonyesha kile kilichotokea.

Kwanza kabisa jukwaa lililo wazi

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Maandalizi

Matayarisho ya mwisho mwisho yalifanywa kwa zulia jekundu kwenye hoteli ya Capella katika kisiwa cha Sentosa huku bendera za Korea Kaskazini na Marekani zikiwa nyuma. Ni nadra kuona bendera za Korea Kaskazini na Marekani zikiwa pamoja na ni ishara ya ushindi mkubwa kwa Kim kuonyesha kuwa nchi hizi mbili zimekuja pamoja zikiwa sawa.

Wote wanaingia jukwaani kutoka pande tofauti

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wakiingia Jukwaani

Kama waliokuwa wamefanya mazoezi kuhusu hili, Trump aliingilia upande wa kulia huku Kim akiingilia upade wa kushoto

Kusalimiana kwa mikono kulidumu sekunde 12

Haki miliki ya picha AFP

"Nimefurahi kukutana nawe Bw Rais," ni maneno aliyoyatamka Bw Kim alipokutana na Bw Trump

Walisaliamiana kwa mkono kwa muda lakini muda walishikana mikono ulikuwa mfupi kuliko ule wa kawaida wa Trump.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kisha Trump anaonekana akimwelekeza Kim

Kisha Trump anaonekana akimwelekeza Kim kutoka kwa zulia ishara kwamba alikuwa akidhibiti hali.

Mazungumzo

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wawili hao walionekana hao wakizungumza kabala ya kuelekea kwa mkutano wa ana kwa ana.

Wawili hao walionekana hao wakizungumza kabala ya kuelekea kwa mkutano wa ana kwa ana.

Wakati huo ulionekana wa kuchanganyikiwa kwa kuwa Kim alionekana akiangalia chini na Bw Trump akiweka pamoja mikono yake.

Akiongoza wakati wa kutembea

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Trump na Kim wakitembea na Trump akiwa hatua mbele kidogo wakielekea kwa mkutano wa moja kwa moja uliodumu dakika 40.

Trump na Kim wakitembea na Trump akiwa hatua mbele kidogo wakielekea kwa mkutano wa moja kwa moja uliodumu dakika 40.

Kwa Trump sasa huenda akajipongeza kuwa mafanikio hayo yametokana na shinikizo zake kwa Korea Kaskazini. Kwa Kim kuweza kukutana na kufanya mazunguznoa na Rais wa Marekani ni ushindi mkubwa.

Siku ya kusalimiana wa mikono mara nyingi

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Wote wakati wa kumalizika kwa mazungmzo ya pamoja na wakati walitoa taarifa ya pamoja kwa waandishi wa habari walisalimiana mara kadhaa.

Wote wakati wa kumalizika kwa mazungmzo ya pamoja na wakati walitoa taarifa ya pamoja kwa waandishi wa habari walisalimiana mara kadhaa.

Ikiwa ni kama ishara ya uhusiano na mambo mazuri bila ya kutojulikana wazi ni kipi walikubaliana.