Kwa nini watu wazima hawazeeki nchini Japan?

Vijana wa Japan watakuwa na majukumu zaidi lakini sio wote Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Vijana wa Japan watakuwa na majukumu zaidi lakini sio wote

Utu uzima huja mapema katika maisha kwa wengi nchini Japan.

Serikali imewasilisha muswada unaopunguza umri wa kuingia utu uzima kutoka miaka 20 hadi 18 , ambao utaathiri mamilioni nchini humo wakati utakapoidhinishwa 2022.

Ni mara ya kwanza umri wa kuwa mtu mzima umebadilishwa tangu ulipoanzishwa 1876.

Je ni nini vijana wenye umri wa miaka 18 wataruhusiwa kufanya ?

Mabadiliko makubwa ni kwamba wataruhusiwa kuolewa ama kuoa bila ruhusa ya wazazi wao.

Kwa sasa, vijana wanaume walio katika umri wa miaka 18 na wasichana wenye umri wa miaka 16 na juu yake wanaweza kuoa au kuolewa lakini baada ya ruhusa ya wazazi wao .La sivyo utalazimika kufikisha umri wa miaka 20.

Llakini sheria inayobadilishwa inaongeza umri ambao wanawake wanaweza kuolewa na inamaanisha kwamba vijana wenye umri wa miaka 18 wataweza kuoa ama kuolewa bila ruhusa ya wazazi wao.

Pia wataweza kutuma maombi ya kutaka kadi za kuomba mkopo bila ya ruhusa ya wazazi, na iwapo wanataka wanaweza kupata cheti cha kusafiria cha miaka 10.

Kwa sasa wavulana na wasichana wanaruhusiwa kuwa na vyeti vya kusafiria kama pasipoti kwa kipindi cha miaka mitano na watahitaji saini ya mzazi ama msimamizi.

Ikiwa miongoni mwa kupunguza umri wa utu uzima , mabadiliko yamefanyiwa sheria 20 , ikiwemo kuhusu uraia. Wale ambao wamepatikana na tatizo la utambulisho wa jinsia wataruhusiwa kuwasilisha ombi la kubadilisha jinsia zao wakiwa na umri wa miaka 18.

Ni nini ambacho hawataruhusiwa kufanya?

Ijapokuwa wameingia katika umri wa utu uzima vijana walio na umri wa miaka 18 nchini Japan hawataruhusiwa kunywa pombe , kuvuta sigara , kucheza kamari na kuasi watoto

Watalazimnika kusalia hadi pale watakapokuwa na umri wa miaka 20 kufanya hivyo .

Mitandao ya kijamii inasemaje kuhusu hilo?

Wengi katika mitandao ya kijamii hawafurahii kuhusu muswada huo mpya.

"Kwa hivyo nitakuwa na umri wa miaka 18 na mtu mzima lakini sitaweza kunywa pombe ama kucheza kamari? aliuliza mtumizi mmoja wa mtandao wa Twitter. ''hilo haliingi akilini''

"Naweza kuchukua mkopo nikiwa na umri wa miaka 18 , lakini kunywa pombe sitaruhusiwa'' , mtumiaji mwengine alisema.

Wengine walisema kuwa kutakuwa na mkanganyiko wakati wa sherehe za kuingia katika utu uzima kila mwaka kwa wale waliofikisha umri wa miaka 20

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Sherehe ya kuwakaribisha vijana kuingia umri wa utu uzima husherehekewa kila Jumatayu ya pili ya mwezi Januari.

Kwa nini mabadiliko hayo yanafanyika?

Kumekuwa na mjadala kuhusu umri wa kuingia utu uzima nchini Japan kwa miongo kadhaa na wizara ya haki mwaka 2009 ilitoa ripoti ikiunga mkono umri wa kuingia utu uzima kupunguzwa hadi 18.

Wanachama wa chama tawala cha LDP wanasema kuwa kupungzwa kwa umri huo kutasaidia kuimarisha jamii inayozeeka ukiangazia kiwango cha chini cha watoto wanaozaliwa.

Mwaka 2015, serikali ilipunguza umri wa kupiga kura kutoka 20 hadi 18.

Mada zinazohusiana