Marekani inaitaka Korea Kaskazini kuangamiza silaha ifikapo 2020

North Korea's leader Kim Jong Un is seen with an intercontinental ballistic rocket in this undated photo released by North Korea's Korean Central News Agency (KCNA) in Pyongyang 30 November 2017.

Chanzo cha picha, KCNA

Maelezo ya picha,

Vyombo vya habari nchini Korea Kaskazini vemrchapisha picha kuinyesha silaha za nchi hiyo

Marekani ina matumaini ya kuanza kuona shughuli ya kuangamizwa silaha nchini Korea Kaskazini ifikapo mwaka 2020, mwa mujibu wa waziri wa mashauri ya nchi za kigeni Mike Pompeo.

Matamshi yake aliyoyatoa alipofanya ziara nchini Korea Kusini, yanafuataia mkutano kati ya Rais Donald Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un.

Walisaini makubaliano ya kufanya kazi katika kuangamiza kabisa silaha za nyuklia katika rasi ya Korea.

Lakini nakala hiyo imekosolewa kwa kukosa taarifa za kina kuhusu ni lini na ni vipi Korea Kaskazini itaachana na silaha zake.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Mike Pompeo (kulia) akiwa Seol

Bw Pompeo alisafiri kutoka Singapore kwenda Seoul ambapo alikuwa akihifahamisha serikali ya Korea Kusini kuhusu matokeo ya mkutano huo.

Alsema bado kuna kazi nyingi ya kufanywa na Korea Kaskazini, "ya kuangamiza silaha ... Tuna matumaini kuwa tutaweza kutimiza hilo ndani ya miaka miwili unusu."

Alisema ana uhakika kuwa Pyongyag ilikuwa inafahamu kuwa shughuli yoyote ya kuangamiza programu yake za nyuklia itahitaji hakikisho.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Trumop akiwasili nyumbani baada ya mkutano na Kim

Rais Trump mapema alitangaza kuwa Korea Kaskazini sio tena tisho la nyuklia akisisitiza kuwa kila mtu sasa anaweza kuhisi salama.

Kipi kiliafikiwa kwenye mkutano huo?

Viongozi hao walisema watashirikana katika kujenga uhusiano mpya huku Marekani ikiihakikishia usalama Korea Kaskazini.

Pyongyan nayo itajitolea katika kuangamzia silaha za nyuklia kwenye rasi ya Korea.

Kisha kwenye mkutano na waandishi wa habari Trump akasema kuwa ataiondolewa Korea Kaskazini vikwazo wakati suala la silaha za nyuklia litatatuliwa.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Marekani hufanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi na Korea Kusini na pia Japan

Alisema anaamini kuwa Bw Kim atatekeleza yale ambayo ameyasema.

Alitangaza kusitishwa mazoezi ya kijeshi ambayo hufanyika mara kwa mara kati ya wanajeshi wa Marekani na Korea Kusini katika rasi wa Korea

Hatua hiyo imekuwa ikiitishwa kwa muda na Pyongyang na ilitangazwa bila matarajio kutoka kwa washirika wa Marekani na iliwapata kwa mshangao.

Makao rasmi ya rais wa Korea Kusini ya Blue House baadaye yalisema yalitaka kufahamu maana kamili ya matamshi ya Trump kuhusu kusitisha mazoezi ya kijeshia ya pamoja.