Sheria ya maudhui ya mitandao zilivyoathiri wenye blogu Tanzania
Huwezi kusikiliza tena

Kanuni za maudhui ya mitandao zilivyoathiri wenye blogu Tanzania

Wanahabari na wadau mbalimbali wamekutana mjini Dar es Salaam ambapo suala la Kanuni za Maudhui ya zimeonekana kuwa mwiba kwa wengi wa watoa huduma za maudhui ya mtandao.

Kanuni hizo zilipitishwa na serikali mwezi Februari mwaka huu ili kudhibiti matumizi na utoaji wa maudhui ya mtandao.

Lakini wanaharakati mbali mbali wamezilalamikia kuwa ni kandamizi kwa uhuru wa habari nchini humo.

Regina Mziwanda amezungumza na baadhi ya wamiliki wa blogu zilizofungiwa na kuandaa taarifa ifuatayo.