Uhispania yawapokea wahamiaji waliokataliwa Italia na Malta

Wahamiaji wamekuwa kwenye meli kwa zaidi ya wiki moja Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wahamiaji wamekuwa kwenye meli kwa zaidi ya wiki moja

Bandari ya Valencia nchini Uhispania imepokea meli ya kwanza iliyokuwa imebeba wahamiaji waliookolewa kutoka kwenye bahari ya Mediterrania na kukataliwa kuingia Italia na Malta.

Meli tatu za kwanza ziliingia bandarini baada ya uda wa alfajiri.Baadhi ya wahamiaji kati ya 629 waliokolewa karibu na nchi ya Libya mwishoni mwa juma lililopita na meli ya Aquarius walianza kuingia.

Maafisa wa kitabibu na watafsiri wa lugha wamesema wako tayari kutoa usaidizi.

Wahamiaji wasababisha Italia kufuta ziara ya waziri wake Ufaransa

Serikali mpya ya kisoshalisti ya Uhispania imeahidi kuwapa huduma za afya bure na kuwa itafanyia uchunguzi kila anayeomba hifadhi.

''Ni jukumu letu kusaidia kuepuka majanga ya kibinaadamu na kutoa msaada wa kuwapatia mahali salama, tukifuata makubaliano ya kimataifa ya kuwa na jukumu la kulinda haki za binaadamu'', Waziri mkuu wa nchi hiyo,Pedro Sánchez alieleza mwanzoni mwa juma hili.

Meli ya doria ya Italia, iliingia kwenye bandari ya Valencia ikiwa na wahamiaji 274, Shirika la habari la Italia, Ansa liliripoti.

Wafanyakazi wa shirika la msalaba mwekundu 1000 walikuwa tayari kuwapokea wahamiaji walipokuwa wakiteremka kutoka kwenye meli.Walikuwepo pia maafisa wa polisi kusaidia katika mapokezi hayo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Meli iitwayo the Dattilo ilikuwa ya kwanza kuwasili

Meli ya pili , the Orione na nyingine ya Aquarius zimekuwa zikitarajiwa asubuhi ya jumapili zikiwa na wahamiaji waliobaki.

Maafisa wanasema wahamiaji waliookolewa wanahusisha watoto 11 chini ya umri wa miaka 13 na wanawake saba wajawazito.

Serikali ya Italia ilikataa meli ya Aquarius kutia nanga nchini humo, Waziri wake wa mambo ya ndani Matteo Salvini akisema kuwa si haki kubeba jukumu hilo , akitaka Malta ipokee wahamiaji hao, Malta nayo ikilikataa jukumu hilo.

Image caption Wahamiaji wamekuwa wakitembea majini kwa muda mrefu kutafuta hifadhi katika mataifa ya Ulaya

Mayor wa Valencia Joan Ribo amesema uamuzi wa Italia wa kukataa meli kuingia nchini mwake ni kitendo kisicho cha kibinaadamu.

ameiambia BBC kuwa ana matumaini kuwa uamuzi wa mji wa Valencia utakuwa ni kama ''mshtuko wa umeme'' na kutia msukumo kufanyia mabadiliko sera za uhamiaji za Umoja wa Ulaya.

Awali, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron aliishutumu Italia kwa kutowajibika na kwa kuifukuza meli ya Aquarius.Serikali yake imesema itaisaidia Uhispania katika kuwashughulikia wahamiaji.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Wahamiaji wengi waliookolewa walikuwa wamedhoofu kutokana na misukosuko ya baharini

Wahamiaji wametumia saa 20 wakiwa kwenye chombo cha majini dhaifu kabla ya kuokolewa.Baada ya hapo walitumia wiki nzima ndani ya meli iliowaokoa, wakiwa kwenye bahari yenye misukosuko wengi wao wakiwa wagonjwa.

kubadilishwa kwa sera za uhamiaji pengine inaweza kuwa moja kati ya ajenda muhimu zitakazojadiliwa katika mkutano wa viongozi wa EU baadae mwezi huu.

Mada zinazohusiana