Maisha ya matumaini katika makazi ya eneo duni la Jalousie nchini Haiti maarufu kwa nyumba zake

Katika nyumba zilizonakshiwa kwa rangi angavu katika eneo duni la Jalousie ambalo ni moja ya maeneo duni nchini Haiti, huishi jamii inayokumbana na changamoto ya kukosa maji safi na maji ya mabomba, umeme na kuishi kwenye rundo la takataka za plastiki.

Muonekano wa eneo la Jalousie kwa mbali Haki miliki ya picha TARIQ ZAID
Image caption Muonekano wa eneo la Jalousie kwa mbali

Zaidi ya watu 80,000 sasa wanaishi Jalousie.Wengi walihamia hapa baada ya tetemeko la ardhi kubwa lililoipiga Haiti mwaka 2010.

Lakini ingawa maisha katika eneo hili yana changamoto kubwa kama vile umaskini na ukandamizaji, wakazi wanajitahidi kuishi kwa utu, matumaini na wanaishi kama jamii nyingine.

Watu wengi wanaotembelea mji mkuu wa Haiti, Port-au-Prince, huliona eneo hili huwa linaonekana kutoka barabarani kutokana na rangi zilizopakwa kwenye makazi hayo

Watoto wakicheza nje ya makazi yao Haki miliki ya picha TARIQ ZAID
Image caption Watoto wakicheza nje ya makazi yao

Nyumba zilipakwa rangi na serikali mwaka 2013 ikiwa ni sehemu ya mradi wa pauni milioni moja, mradi ambao ulikuwa ukidhihakiwa kuwa usio na maana

Wakosoaji wanasema fedha hizo zingetumika katika kuweka miundombinu ya maji na umeme kuliko kupendezesha muonekano wa nyumba za eneo hilo kwa ajili ya hadhi ya wilaya ya P├ętion-Ville.

Nyumba zao zina nakshi ya rangi angavu Haki miliki ya picha TARIQ ZAID
Image caption Nyumba zao zina nakshi ya rangi angavu

Ukifika katika eneo hili duni lenye nyumba zilizobanana hupati shida kuona changamoto walizonazo wakazi wa eneo hili.

Kutokana na nyaya za umeme kuunganishwa kiholela, wakazi wanapata umeme kwa ajili ya kuwasha mkaa kwa ajili ya kupikia, na mvua inaponyesha, maji husafirisha uchafu wa plastiki ambao hunasa nje ya makazi ya watu

Wakazi hufanya bidii kuboresha mazingira yanayowazunguka Haki miliki ya picha TARIQ ZAID
Image caption Wakazi hufanya bidii kuboresha mazingira yanayowazunguka

Pamoja na kuwepo kwa hali ya umaskini uliokithiri wakazi wa Jalousie wanafanya kazi kwa bidii kwa ajili ya kuboresha hadhi yao na mazingira yanayowazunguka.

Wanatengeneza maeneo ya muda mfupi kwa ajili ya kufanya mazoezi wakibeba vitu vizito vilivyotengenezwa na saruji, pia huenda kwenye moja ya makanisa yaliyo katika eneo hilo

Shughuli mbalimbali za kimichezo zinaendelea Haki miliki ya picha TARIQ ZAID
Image caption Shughuli mbalimbali za kimichezo zinaendelea
Watu huhudhuria ibada kanisani Haki miliki ya picha TARIQ ZAID
Image caption Watu huhudhuria ibada kanisani
Watoto wakicheza Haki miliki ya picha TARIQ ZAID
Image caption Watoto wakicheza

Watu wa Jalousie wanafanya biashara hapo hapo kama biashara ya shughuli za urembo na migahawa ili kujipatia kipato.

Wafanya biashara ya urembo wanajipatia kipato pia Haki miliki ya picha TARIQ ZAID
Image caption Wafanya biashara ya urembo wanajipatia kipato pia
Moja ya familia ya Jalousie Haki miliki ya picha TARIQ ZAID
Image caption Moja ya familia ya Jalousie

Loreu,62 ana duka analouza mkaa. Baba wa watoto wanne amekuwa akiishi Jalousie kwa zaidi ya miaka 40

Mfanya biashara wa mkaa Haki miliki ya picha TARIQ ZAID
Image caption Mfanya biashara wa mkaa

Pamoja na jitihada zao asilimia 85 ya familia za eneo hilo wanasema kipato chao kinakidhi sehemu ndogo tu ya mahitaji yao

Jean Michelle, 35, anafanya kazi ya ulinzi kwenye maegesho ya magari anaishi kwenye chumba kimoja akiwa na watoto wake watatu tangu mwaka 2004.

Hapa, anamsaidia binti yake Fatdjoulie kazi ya shule huku Catrine Telamoure anayeishi pamoja nao akiwa amelala.

Baba akifanya kazi za shule na binti yake Haki miliki ya picha TARIQ ZAID
Image caption Baba akifanya kazi za shule na binti yake

Haiti ni taifa masikini limekuwa likipambana kujinasua na athari za tetemeko la ardhi la mwaka 2010 lililosababisha vifo vya watu 200,000

Utafiti wa hivi karibuni unasema watu wake wanaishi kwa kiasi cha dola 2.41 kwa siku.asilimia 74 ya watu waliokuwa wakiishi mjini sasa wanaishi kwenye vitongoji duni.

Wakazi hawa hubeba ndoo za maji za lita 20 kichwani Haki miliki ya picha TARIQ ZAID
Image caption Wakazi hawa hubeba ndoo za maji za lita 20 kichwani

Kutokana na kukosa umeme, wakazi wa Jalousie hawana maji ya bomba.

Wakazi hupanga mstari katika vituo vya kusambaza maji wakilipia dola 0.35 kwa ndoo ya lita 20.

Kuna hatari ya kutokea maporomoko Haki miliki ya picha TARIQ ZAID
Image caption Kuna hatari ya kutokea maporomoko

Kuna hatari ya kutokea kwa maporomoko, kutokana na miteremko iliyopo na kukosekana kwa uoto, nyumba zisizo imara 1,300 ni tishio kwa wakazi wa eneo hilo.

Mada zinazohusiana