Wachezaji wa Saudi Arabia wanusurika na ajali ya ndege Urusi

Ndege ya Kampuni ya Rossia
Image caption Ndege ya Kampuni ya Rossia

Ndege iliyowabeba wachezaji wa timu ya taifa ya Saudi Arabia kuelekea kusini mwa Urusi, kwa michuano inayoendelea imetua salama baada ya kupata hitilafu katika moja ya injini ya ndege hiyo baada ya moto kutokea.

Picha za video zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinaionyesha ndege hiyo katika chini ya bawa lake kukiwa na cheche za moto.

Ndege hiyo ya shirika la Rossiya ilipatwa na shida hiyo wakati ikitua uwanja wa Rostov-on-Don.

Shirikisho la mpira la Saudia,limesema kuwa wachezaji wote wapo salama.

Mchezaji kiungo wa Saudi Arabia Atan Bahbir,na mchezaji katika nafasi ya ulinzi Osama Hawsawi,wanasema wanamshukuru Mungu kwa kuwafikisha salama.

"Tunashukuru kwa swali lako, tunamshukuru Mungu,msafara mzima umefika salama. Kulikuwa na shida ya kiufundi, na tulipatwa na uoga kidogo.

Haki miliki ya picha BBC Sport
Image caption Wachezaji wa Saudia wakishuka salama kwenye ndege

Naye mchezaji Osama amesema kuwa wanashukuru Mungu kuona kwamba sasa wapo hotelini, kwani kwa sasa kila kitu kipo sawa, na amesema wanamuomba Mungu washinde katika mchezo wao.