Nduguye mchekeshaji Eric Omondi kutoka Kenya aaga dunia

Nduguye Eric Omondi Haki miliki ya picha Eric Omondi/facebook

Nduguye msanii mchekeshaji kutoka Kenya Eric Omondi amefariki saa chache baada ya kupatikana na familia yake katika jumba moja Nairobi, baada ya kutafutwa kwa muda.

Joseph Omondi Erick alipatikana katika hali mbaya ya kiafya bada ya kipindi kirefu cha matumizi wa mihadarati kabla ya kuaga dunia mapema leo alfajiri.

''Hii sio picha ambayo ningependa kuchapisha , lakini hii ndio picha ambayo ningependa kila kijana katika taifa hili kuona. Joseph Onyango Omondi alifariki saa 12 baada ya kumpata katika eneo la River Road. Alikuwa mtumizi wa Cocaine na madawa mengine na alikuwa akipelekwa na kutolewa katika taasisi za kubadilisha tabia kwa kipindi cha miaka 19 iliopita. Mungu ndiye muamuzi'', aliandika Eric kwenye Instagram.

Mcheshi huyo anasema kuwa alimtafuta nduguye baada ya kuelezewa aliko na dereva wa teksi katika barabara ya Nyandarua jijini Nairobi.

Aliandika katika akaunti yake ya Instagram na kuelezea vile nduguye alivyotatizika na utumizi wa mihadarati tangu shule ya upili.

''Iwapo wewe ni kijana mdogo na unafuata akaunti hii, huu ujumbe ni wako!!! huyu ni ndugu yangu mkubwa mama mmoja baba mmoja. Joseph amekuwa na tatizo la utumizi wa mihadarati tangu shule ya upili, amekuwa ndani na nje ya taasisi za kurekebisha tabia, sisi kama familia tumejaribu uwezo wetu wote'', aliandika.

Vile vile amewashauri vijana waliopo shuleni na ambao wanatumia mihadarati kuwacha tabia hiyo.

''Kutokana na tatizo lake la utumizi wa mihadarati, amekuwa na tabia ya kututoroka ili kukwepa kupelekewa katika taasisi za kubadilishia watumizi wa mihadarati tabia.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii