Kwa nini watu wanasambaza sana picha hii?

Justin na Aminat McClure wapaiga picha wakiwa wamevalia nguo za magharibi mwa Afrika pamoja na watoto wao watatu Haki miliki ya picha Justin McClure
Image caption Justin na Aminat McClure wapaiga picha wakiwa wamevalia nguo za magharibi mwa Afrika pamoja na watoto wao watatu

Picha za familia mara nyingi huwavutia watu wengi katika mitandao ya kijamii , lakini hii imewavutia watu, kuisambaza na kuipenda zaidi.

Wanandoa wa Marekani Aminat na Justin McClure walichapisha picha hii ili kusherehekea familia ilio na mchanganyiko wa tamaduni , hatua iliosababisha maelfu ya watu kuisambaza , wengi wao wakitoka katika familia zenye tamaduni tofauti.

Wanandoa hao wanaoishi mjini New Jersy , Marekani walipiga picha hiyo pamoja na watoto wao wakiwa wamevalia nguo yenye mtindo wa Afrika magharibi ili kuheshimu tamaduni ya Nigeria ambako Aminata anatoka.

Aliondoka Lagos , kusini magharibi mwa Nigeria wakati familia yake iliopoelekea Marekani akiwa mdogo.

"Tulitaka kuwapatia watoto hawa funzo kuhusu tamaduni tofauti zilizopo duniani ili kuweza kujinufaisha kwa kuzikubali', Justin aliambia BBC.

"Kama familia tungependa kuweka taarifa yenye uzito na ningependa kusherehekea utamaduni wa Aminata.

Nguo hizo zilishonwa na mwanamitindo mmoja kutoka Cameroon Claude Kameni, ambaye aliwasiliana na familia hiyo akitaka kuwatengezea nguo hizo.

Wanandoa hao ambao wanawao pacha ni maarufu sana katika mitandao ya kijamii walichapisha picha hiyo katoka mtandao wa instagram na facebook ambapo imesambazwa mara 15,000 .

Chapisho hilo lenye kichwa kikuu ''Sherehekeeni tamaduni zenu na pia tamaduni za wale munaowapenda, nani anunga mkono wazo hili? imezungumziwa zaidi ya mara 2,200

Mwanamke mmoja ambaye aliishukuru familia hiyo kwa kuonyesha tamaduni tofauti , alielezea kwamba pia yeye anatoka familia ilio 'na rangi tofauti'.

Haki miliki ya picha Renita Cleaver

Wengine walivutiwa na kupata msukumo mbali na kusambaza matumaini yao ya kuwalea watoto waliozaliwa kutoka baba na mama walio na tamaduni tofauti ikiwemo lugha.

"Hii ni nzuri sana, aliandika mtumiaji mmoja wa ukurasa wa facebook Aber Rose Luna. Mimi ni mwanamke mwenye mizizi ya Marekani na Itali na mume wangu ni Mexicana.

''Mimi mwenyewe hupendelea wana wangu wawe wanaweza kuzungumza lugha ya Kihispania na Kiingereza kwa sababu sipendi tamaduni zao za Mexican kupotea kwa sababu sijui lugha hiyo''.

Wengine walikumbuka sherehe za kifamilia ambazo zilikuwa na mchanganyiko tofauti wa tamaduni.

"Naipenda picha hii , aliandika Liz Poma. "Ndugu yangu aliolewa na mkewe anatoka Ghana. Mkewe alituuliza iwapo tungependelea kuvaa nguo za taifa lake kwa sababu walitaka tujihisi kwamba tunashirikishwa. Sasa watoto wake wa kike wanafunzwa kukubali tamaduni zote mbili.

Haki miliki ya picha Liz Poma

Picha hiyo pia ilirudisha kumbukumbu za mwanamke mmoja ambaye alikuwa na wazazi kutoka tamaduni tofauti.

''Mamangu ni mweupe, aliyeolewa na raia wa Nigeria na huvalia nguo za Nigeria kila mara. Amekumbatia tamaduni yake sana mpaka akajivunza kupika chakula cha Nigeria anachokipenda na vilevile kujifunza kuzungumza lugha hiyo'', alisema Angela Ansaldi.

Kwa familia ya McCluster sio mara ya kwanza kwamba wamefanya juhudi za kujua tamaduni za Aminata pamoja na watoto.

Wametembelea migawaha ya Nigeria kupika chakula kama vile Puff Puff pamoja na watoto.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii