Canada sasa ruhusa matumizi ya bangi hadharani

Bangi sasa halali Canada

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Bangi sasa halali Canada

Canada imepitisha sheria rasmi kwa nchi nzima inayoruhusu matumizi ya bangi.

Sheria hiyo hatimaye ilishinda kwa kupata kura za ndiyo 52 zinazoruhusu matumizi ya bangi hadharani,huku kura 29 za maseneta zikisema hapana.

Sheria hiyo inasimamia udhibiti,usambazaji na uuzaji wake.

Chanzo cha picha, AFP/GETTY

Maelezo ya picha,

Raia wa Canada wataruhusiwa kununua na kutumia bangi kihalali kuanzia mapema mwezi Septemba

Kwa sheria hiyo sasa raia wa Canada wataruhusiwa kununua na kutumia bangi kihalali kuanzia mapema mwezi Septemba mwaka huu.

Kumiliki bangi ilikuwa ni kosa kisheria tangu mwaka 1923 lakini matumizi ya bangi kama dawa yaliruhusiwa kisheria tangu mwaka 2001.

Kutokana na kupitishwa kwa sharia hiyo sasa itawachukua majimbo,Manispaa na mamlaka takribani wiki kati ya nane hadi 12 kutengeneza masoko mapya ya kuuza bangi.

Lakini pia muda huu kabla ya kuanza kutumika kwa bangi rasmi,utatumika na Polisi kuandaa mifumo mipya ya kisheria.

Kwa mjibu wa sheria hii mpya mtu ataruhusiwa kuagiza bidhaa hii ya bangi kwa mfumo wa kimtandao kutoka kwa wasambazaji wanaotambulika kisheria.

Chanzo cha picha, PRESS ASSOCIATION

Maelezo ya picha,

Watu nchini Canada ni baadhi ya watumiaji wakubwa wa bangi duniani.

Watu wazima wataruhusiwa kumiliki hadharani hadi gram 30 ya bangi kavu hadharani.

Umri unaoruhusiwa kununua na kutumia bangi umepitishwa kwa mjibu wa sharia hiyo kwamba ni kuanzia miaka 18,lakini baadhi ya majimbo yamependekeza umri wa kuanzia miaka 19. Ni

Ni kwa nini Canada ifanya hili sasa?

Sheria hiyo inahitimiza ahadi ya kampeni ya Bw Tudeau, kioongozi wa chama cha Liberal.

Waziri huyo mkuu amesema kuwa sheria za miaka mingi za Canada zinazoharamisha matumizi ya bangi hazina maana kwa kuwa watu nchini Canada ni baadhi ya watumiaji wakubwa wa bangi duniani.

Kura za maoni zimekuwa zikionyesha kuwa watu wengi nchini Canada wanaunga mkono hatua hiyo.

Hatua ya kuhalalisha matumizi ya bangi kwa burudani nchini Canada yanakuja wakatoi nchi za dunia zinahalalisha bangi inayotumiwa kwa kiwango kikubwa duniani.