Panya wavamia mtambo wa ATM na 'kutafuna' pesa nchini India

Rats eat grains of rice in Allahabad, India, on July 28, 2015 Haki miliki ya picha Getty Images

Mafundi waliofika kuukarabati mtambo wa ATM ambao ulikuwa umeharibika katika jimbo moja nchini India walipigwa na butwaa walipoufungua kubaini tatizo lilikuwa wapi.

Noti za thamani ya rupia 1.2m (£13,300; $17,600) zilikuwa zimechanwa na kuraruliwa na panya katika benki hiyo jimbo la Assam.

Polisi wanasema panya hao pengine waliiingia ndani ya mtambo huo kwa kupitia kwenye tundu lililokuwa litumiwe kuingizia nyaya, gazeti la Hindustan Times limeripoti.

Picha zinazoonesha pesa zilizokuwa zimetafunwa na panya hao katika mtambo huo wa Benki ya Dola ya India katika wilaya ya Tinsukia zimesambazwa sana kwenye Twitter.

Moja inaonesha mzoga wa mmoja wa panya hao kwenye mabaki ya noti hizo.

Afisa wa polisi Prakash Sonowal alisema kwamba mtambo huo umekuwa haufanyi kazi kwa siku 12 hizi, gazeti la Hindustan Times limeongeza.

Mafundi waliofungua mtambo huo walipata noti za rupia 2,000 na rupia 500 zikiwa zimeharibiwa.

Walifanikiwa kunusuru noti za jumla ya thamani ya rupia 1.7 milioni, maafisa wanasema.

Unaweza kusoma pia:

Mada zinazohusiana