Kwa Picha: Wanawake wanavyojiandaa kuendesha magari Saudia

Huku Saudia ikijiandaa kusitisha ,marufuku ya kendesha gari miongoni mwa wanawake tarehe 24 mwezi June, kampuni ya mafuta ya serikali Aramco imejitolea kuwafunza wafanyikazi wake wa kike kuendesha gari.

Mpiga picha wa Reauters Ahmed Jadallah na ripota Rania El Gamal walijiunga na baadhi ya wanawake 200 wanaofunzwa katika taasisi ya mafunzo ya kuendesha magari ya Aramco Driving Center mjini Dhahran.

Chanzo cha picha, Reuters

Mmoja ya wanafunzi hao ni Maria al-Faraj (aliyepigwa picha chini), ambaye anapatiwa mafunzo na mwalimu wake Ahlam al-Somali.

Chanzo cha picha, Reuters

Mbali na kufunzwa kuendesha gari, pia anafunzwa kuangalia kiwango cha mafuta , kubadilisha matairi na umuhimu wa kufunga mshipi katika kiti.

Chanzo cha picha, Reuters

Chanzo cha picha, Reuters

Chanzo cha picha, Reuters

Chanzo cha picha, Reuters

Kuondolewa kwa marufuku hiyo ni ufanisi mkubwa miongoni mwa wanawake nchini Saudia.

Awali walikuwa wakipigwa faini ama hata kukamatwa iwapo watapatikana wakiendesha magari, na walikuwa wakitegemea watu wa familia zao kuwaendesha badala yake.

Chanzo cha picha, Reuters

Amira Abdulgader (kwenye picha chini} anasema kwamba tarehe 24 mwezi Juni anapanga kuwa katika usukani akimbeba mamake.

Chanzo cha picha, Reuters

Chanzo cha picha, Reuters

"Kuendesha gari kunamaanisha wewe ndio unadhibiti munakoelekea,," Amira Abdulgader alisema.

"Mimi ndio nitaamua wakati wa kwenda na wakati nitakaporudi''

"Tunahitaji gari kufanya shughuli za kila siku. Tunafanya kazi sisi ni akina mama, tuna watu wengi wa kutembelea , tunahitaji kwenda kujivinjari-hivyobasi tunahitaji uchukuzi. itabadilisha maisha yangu''.

Chanzo cha picha, Reuters

Wanawake ni asilimia 5% ya wafanyikazi wa Aramco walio 66,000-, ikimaanisha kwamba wengine 3000 wanaweza kuanza kujifunza kuendesha gari kulingana na Reuters .

Chanzo cha picha, Reuters

Ijapokuwa Saudia imepongezwa kwa kuamua kuondoa marufuku ya wanawake kuendesha gari , haijaikosa utata.

wanaharakati ambao wamekuwa wakipigania marufuku hiyo kuondolewa wanasema kuwa wamepokea vitisho vya mtandaoni , huku baadhi yao wakikamatwa mnamo mwezi Mei kwa shauku ya kuwa wasaliti ambao wanashirikiana na serikali za kigeni.

picha kwa niaba ya Ahmed Jadallah.