Mkimbizi kutoka Burundi anayefanikiwa katika kilimo kambini Kakuma, Kenya

Mkimbizi kutoka Burundi anayefanikiwa katika kilimo kambini Kakuma, Kenya

Ufadhili kwa wakimbizi unaendelea kukumbwa na changamoto huku idadi ya waliolazimika kukimbia vita ikiendelea kuongezeka kote duniani.

Takwimu za Umoja wa mataifa zinaonesha kuwa watu wapatao milioni 68 wamelazimika kuhama makwao mwanzoni mwa mwaka huu.

Katika juhudi za kuwapa wakimbizi uwezo wa kujisimamia, mradi maalum wa kilimo unaendeshwa katika kambi ya Kakuma kaskazini mwa Kenya. Nzeyimana Alphoncine kutoka Burundi ni mmoja wa waliofanikiwa.

Video: Kenneth Mungai, BBC