Je bangi inaweza kuwa tiba katika penzi lililozorota?

Mchango wa bangi katika mapenzi ya watumizi wawili Haki miliki ya picha Raphaelle Martin
Image caption Mchango wa bangi katika mapenzi ya watumizi wawili

Adam na Dounia kutoka mji wa Luton, Uingereza wamekuwa wakitumia bangi kabla ya kushiriki tendo la ndoa kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

Mara nyingine hutumia bangi ili kuondoa hali ya wasiwasi katika chumba chao cha kulala, alielezea Dounia.

Anasema kwamba yeye hutumia marashi yaliochanganywa na bangi katika sehemu zake za siri ili kujipatia joto, kitu ambacho hawezi kuishi bila kufanya .

Huku Canada ikihalallisha utumizi wa bangi -likiwa taifa la pili la pekee kutengeza bidhaa kutokana na mmea huo baada ya Uruguay- nayo serikali ya Uingereza ikitaka kufanyia marekebisho sheria kuhusu utumizi wa bangi kama tiba, watu wanaangazia masuala mengine muhimu ambayo mmea huo unaweza kutoa.

Adam na Dounia ni miongoni mwa idadi ya watu, inayozidi kuongezeka, wanaotumia bidhaa za bangi wakati wa kujamiiana kwa lengo la kuongeza 'mahanjam'.

''Sijiamini, sina mwili mzuri unaovutia'', alisema Dounia. "Lakini bangi inanisaidia kusahau fikira kama hizo na kufanya mwili wangu na akili yangu kutulia, kupitia kuchoma mishumaa iliotengezwa na bangi katika chumba changu".

Kulingana na historia bangi, idaiwa kutoa usaidizi mkubwa chumbani.

Image caption Baadhi ya wavutaji wa bangi

Kwa mfano Wahindi wanaamini kwamba kinywaji cha bangi kinapandisha mihemko ya kutaka kufanya ngono, huku Wamisri wa zama za kale wakidaiwa kutumia bangi iliochanganywa na asali katika sehemu zao za siri ili kupunguza joto lililopo katika kizazi chao.

Na sasa huku sheria kuhusu utumizi wa bangi zikiendelea kulegezwa, idadi ya watu wanaotumia bidhaa za mafuta ya masaji, marashi mishumaa na maua yanayotengezwa kutokana na bangi inazidi kuongezeka.

Neno 'Cannasexual' lilianzishwa na mshauri wa masuala ya ngono Ashley Manta kutoka California 2013 ambaye alianzisha mafunzo ya ngono kutokana na mmea huo wa bangi.

Anaelezea: "Ninawashauri watu kuimarisha maisha yao ya ngono kwa kutumia mmea wa bangi. Kwa kawaida, hii inamaanisha kuwa na mazungumzo ya moja kwa moja na mwathiriwa katika warsha na makundi, mara nyingine kwa kutumia vifaa kuelezea."

Image caption Mtumiaji wa bangi

Warsha hizo huangazia masuala kadhaa ikiwemo ujuzi ama uhodari wako, kuajiamini, mazungumzo machafu na zaidi.

Utumizi wa bangi huangaziwa wakati wote kuhusu ni wapi unaweza kusaidia hususan muda, kiwango na mbinu ya utumizi wake.

"Kimsingi, ni uchanganyaji wa bangi na akili iliyoshawishika kingono wakati wa kuchagua bidhaa unazotaka kutumia mwilini ili kuongeza raha na vitendo vya kimapenzi, na kuongeza faraja na ujasiri," anasema.

Ongezeko la watu wanaotumia bangi katika mapenzi linamaanisha kwamba wafanyibiashara wa bangi nchini Marekani wanadai kwamba wanajaribu kukidhi mahitaji ya bidhaa zinazosababisha mihemko kama vile mafuta yanayopakwa katika sehemu za siri za wanawake.

Wakati Adam na Dounia walipoanza kutumia bidhaa hiyo 2015, Adam tayari alikuwa mtumiaji wa mara kwa mara wa bangi, sana sana alipendelea kutumia kabla ya kufanya mapenzi.

Image caption Wafanyikazi katika kiwanda cha kutengengeza bidhaa za bangi

Ijapokuwa Dounia hakuwa akifanya hivyo, wakati alipokuwa akitafuta mafunzo kuhusu kujiamini mtandaoni, alipata majadiliano yaliomvutia kuhusu kuhusisha bangi katika ngono.

''Nilifuata maelezo niliyopata katika mtandao na kutengeza kiwango kidogo cha mafuta ya bangi ambayo nilitumia. Nilimpeleka Adam chumbani na nikahisi sina wasiwasi tulipoanza kufanya mapenzi''.

Siku hizi Adam huvuta bangi kabla ya kufanya mapenzi, hatua inayomaanisha kwamba hupata 'mshawasha' fulani wa kuwa na hamu ya kushiriki tendo la ngono.

''Mimi uhisi kwamba inanipatia 'mahanjam'', anasema.

Inanipatia nguvu na kudumu muda mrefu wakati wa tendo la ngono.

Hatahivyo itategemea kiwango unachotumia. Unapotumia kiasi kidogo unathirika zaidi.

Hata hivyo mbali na manufaa yanayoletwa na bangi kama anavyodai Adam, utafiti umeonyesha kwamba matumizi wa bangi yanaweza kuathiri uwezo wako wa kutekeleza tendo la ngono miongoni mwa wanaume.

Utafiti uliofanywa na shirika la kijamii la International Society for Sexual Medicine mwaka 2011, ulibaini kwamba kuna athari mbaya kwa tishu za umme miongoni mwa wanyama.

Image caption Bidhaa zinazotokana na bangi

Utafiti mwingine umeonyesha kuwa watu wanaotumia bangi mara kwa mara wana uwezekano wa juu kukabiliwa na tatizo la kusimamisha uume.

Daktari Mark Lawton, mshauri na msemaji wa shirika la Uingereza kuhusu afya ya ngono na HIV, anaamini kwamba watu wanafaa kuchukua tahadhari wakati wa tendo la ngono.

''Masuala kama bangi, ama pombe yanaweza kuathiri maamuzi yetu'', anasema.

Tunajua kwamba mipira ya kondomu kwa mfano haitumiwi na watu wanaotumia dawa wakati wa ngono.

Kuna hatari kwamba baadhi ya maamuzi yanayofanywa chini ya ushawishi fulani yanaweza kuwa tofauti wakati hatujatumia kishawishi chochote.

Daktari Lawton hata hivyo anatambua kwamba huenda bangi ikatumika katika siku zijazo kama kishawishi wakati wa kufanya ngono.

Kuna habari kuhusu baadhi ya bidhaa za bangi ambazo zinaweza kuwa na mafufaa ya kimatibabu, hivyo basi utafiti zaidi utalazimika kufanyika siku zijazo.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii