Kombe la Dunia 2018: Tangazo lililowahimiza wanawake kuzaa na wachezaji wa nje Urusi lashutumiwa

Kaliningrad watches Russia vs Egypt Haki miliki ya picha OZAN KOSE/AFP
Image caption Shabiki wa Urusi akitazama Urusi ilipoichapa Misri

Maduka maarufu ya vyakula nchini Urusi yameomba msamaha baada ya kutangaza zawadi ya dola 47,000 na 'burger' (mkate maalum uliotiwa nyama) maishani kwa mwanamke yeyote ambaye angejamiiana na kuzaa mtoto na mchezaji wa kandanda kutoka nchi za nje katika Kombe la Dunia.

"Mwanamke ambaye atafanikiwa kupata jeni za mchezaji bora zaidi ataisaidia Urusi kupata mafanikio miaka inayokuja," tangazo hilo lilisema.

Tangazo hilo lilizua hisia tofauti nchini Urusi ambayo ndiyo inaandaa Kombe la Dunia hali iliyolazimu kampumi hiyo kulifuta tangazo hilo.

Haki miliki ya picha VKontakte
Image caption Tangazo hilo litangaza zawadi ya pesa na burger kwa wale watazaa na wanasoka

Kwenye matangazo na vyombo vya habari, wanawake wa urusi wanatajwa kuwa wawindani wa ngono.

Makala katika vyombo vya habari vya Urusi yanaandika kuhusu jinsi wanawawinda mashabiki wa kigeni na kuongea nao.

Katika video moja ya YouTube mtangazaji mmoja wa kipindi anasema "maelfu ya wanyonyaji damu" wamefurika Moscow kwa matumaini ya kukutana na mashabiki wa kandanda wa kigeni.

Haki miliki ya picha Telegram
Image caption Mwanamke huyu hakuajua matusi yalielekezwa kwake

Matusi yanayowalenga wanawake hayajibiwi

Wakati video moja iliibuka mitandaoni ikionyesha mashabiki kutoka Brazil wakiimba maneno machafu kwa lugha ya Kireno kwa mwanamke Mrusi na kuzua ghadhabu nchini Brazil lakini hakukuchukuliwa hatua zozote nchini Urusi.

Mwanamke ambaye haifahamu lugha ya Kireno anaonekana akitabasamu akijaribu kuimba na mashabiki hao wa Brazil, bila kuelewa kile walichokuwa wakiimba kuhusu moja ya sehemu yake ya mwili.

Ombi la mtandaoni nchini Urusi la kutaka wahusika kuchukuliwa hatua za kisheria limepata sahihi 2,500.

Baadhi ya wale walihusika wametambuliwa kwenye vyombo vya habari nchini Brazil.