Vijana wanaoteleza kwa viatu vya matairi kupata kipato Tanzania
Huwezi kusikiliza tena

Ilala Skaters: Vijana wanaoteleza kwa viatu vya matairi kupata kipato Tanzania

Umoja wa Vijana wanaocheza mchezo wa kuteleza na viatu vya matairi “Ilala Rollers Skate Society “ Jijini Dar es Salaam nchini Tanzania wanautumia mchezo huu kujipatia kipato licha ya kukabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo ukosefu wa eneo maalumu la kufanyia mazoezi na kuchezea lakini pia mchezo huu una mapokeo hasi Kwa jamiii baadhi wakiuona ni hatari na wanao ucheza ni genge la wahuni.

Vijana Hawa wanakitumia kituo cha daladala cha Moroco kama eneo Lao la mazoezi na ofisi yao pindi wanapohitajika na makampuni na watu binafsi Kwa ajili ya kusambaza vipeperushi na kubandika matangazo.

Video: Eagan Salla, BBC

Mada zinazohusiana