Sara Netanyahu: Mkewe Netanyahu ashtakiwa kwa ulaghai Israeli

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema tuhuma dhidi ya mkewe 'hazina msingi wowote' Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema tuhuma dhidi ya mkewe 'hazina msingi wowote'

Mkewe waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameshtakiwa kwa ulaghai kutokana na madai ya ubadhirifu wa fedha za umma.

Sara Netanyahu ameshtakiwa kwa ubadhirifu wa $100,000 kwa huduma za upishi katika makaazi rasmi ya waziri mkuu.

Bi Netanyahu amekana kufanya makosa yoyote.

Mawakili wake wameyataja mashtaka hayo kama ya kiwendawazimu na yasio na msingi wowote.

Alishtakiwa Alhamisi pamoja na Ezra Seidoff, aliyekuwa mkurugenzi mkuu katika ofisi ya waziri mkuu.

Ofisi ya mwendesha mashtaka imesema imeamua kuwasilisha mashtaka dhidi ya wawili hao baada ya 'kuchunguza ushahidi wote na kupima uzito wa kesi yenyewe'.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Sara Netanyahu amekana mashtaka

Mwaka jana Mkuu wa sheria Avichai Mandelblit alitangaza kuwa anatafakari iwapo amshtaki Bi Netanyahu kuhusu shutuma hizo baada ya uchunguzi wa muda mrefu, ambao umezusha uvumi mwingi katika vyombo vya habari Israel.

Tuhuma ni zipi?

Kwa mujibu wa mashtaka, Bi Netanyahu na bwana Seidoff wanatuhumiwa kwa kuhusika katika matumizi ya fedha katiya Septemba 2010 na Machi 2013 walizotumia kununua chakula kilichopelekwa katika makaazi ya waziri mkuu na pia kuwaajiri wapishi binafsi.

Matumizi hayo yanasemekana kuwa wakati kukifichwa kuwa mpishi aliajiriwa katika makaazi hayo.

Serikali hairuhusu matumizi kwa mambo hayo mawili.

Waziri mkuu Netanyahu amejibu kwa hasira kwa kile ambacho kwa muda mrefu amekiona kuwa kuandamwa kwa familia yake na wanasiasa wa upinzani.

"Sara Netanyahu ni mwanamke mwenye nguvu na heshima, na hajafanya makosa yoyote katika hatua anazochukua," taarifa katika ukurasa wa waziri mkuu wa Facebook ilisema.

Mawakili wa Netanyahu wamesema hakuna ulaghai wowote na hakujua mipangilio.

Mtu aliyeagiza vyakula ni aliyekuwa msimamizi wa makaazi hayo ambaye sasa ni shahidi wa serikali katika kesi, waliongeza.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii