Zaidi ya watu 86 wameuawa katika mapigano ya wakulima na wafugaji Nigeria

Wakulima wakionekana kujihami kwa silaha wakati wa malisho ya mifugo yao
Image caption Wakulima wakionekana kujihami kwa silaha wakati wa malisho ya mifugo yao

Zaidi ya watu 86 wameuawa Katikati mwa nchi ya Nigeria katika muendelezo wa mgogoro kati ya wafugaji na wakulima.

Kwa mujibu wa maafisa wa mji huo, mapigano hayo yalianza siku ya Alhamisi baada ya kundi moja la wakulima kutekwa na watano kati yao kuuawa, kabla ya tukio kubwa linalotajwa kuwa la kulipiza kisasi siku ya Jumamosi dhidi ya wakulima.

Mapigano makali yametokea katika vijiji mbalimbali katikati mwa nchi ya Nigeria ndani ya siku chache, yameacha makovu kwa kusababisha vifo vya watu wengi na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Image caption Mmoja wa wakulima akilinda kijiji chake

Katika eneo la Barkin Ladi mapigano hayo yameshamiri zaidi kiwa ndio eneo ambalo mgogoro umekuwa ukitokea mara kwa mara licha ya kwamba hali ilikua shwari ndani ya miaka miwili iliyopita.

Mapigano yaliripotiwa kutokea tena mwezi April, lakini haya ya sasa yamekithiri.

Watu 31 wauawa kwenye shambulio Nigeria

Uraibu wa Tramadol wachochea machafuko Nigeria

Tokea kuanza kwa mwaka huu, mapigano haya yaliripotiwa kutokea katika baadhi ya maeneo ya katikati mwa Nigeria, licha ya kutajwa kuwa yalizuiliwa na vikosi vya usalama.

Mapigano haya ambayo ni ya kulipizana visasi, licha ya kusababisha vifo vingi sambamba na majeruhi, pia vimesababisha mgawanyiko mkubwa wa ukabila na udini katika eneo hilo.

Polisi nchini Nigeria tiyari imetuma vikosi vyake katika maeneo yaliyoathirika ili kudhibiti hali ya mambo.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii