Mwana wa msanii wa Nigeria D'banj afa maji nyumbani

D'banj
Image caption Mwanamuziki huyo ambaye jina lake kamili ni Oladapo Daniel Oyebanjo, aliitwa baba Mei 2017

Mtoto wa mwaka mmoja wa mwanamuziki nyota wa Nigeria D'banj amekufa maji nyumbani kwao mjini Lagos.

D'banj hakuweza kuthibitisha hadharani kisa hicho lakini alichapisha picha nyeusi kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuandika "Nyakati Ngumu".

Alikuwa huko Los Angeles kuhudhuria sherehe ya tuzo za BET wakati mtoto wake huyo alipokufa.

Mwanamuziki huyo wa Afrobeats alipata umaarufu dunia nzima kutokana na wimbo wake 2012, Oliver Twist.

Haki miliki ya picha iambangalee/ Instagram
Image caption D'banj na mtoto wake

Anajiita "Koko master" jina linaloweza kumaanisha mambo tofauti ikiwemo "bosi", "mpenzi" na "mada kuu ".

Muziki wake ni mchanganyiko wa lugha za Yoruba, Kiingereza na Pidgin.

D'banj, ambaye jina lake kamili ni Oladapo Daniel Oyebanjo, aliitwa baba Mei 2017 na kuchapisha picha za mtoto wake Daniel Oyebanjo III.

Picha yake ya mwisho ilikuwa siku ya baba duniani tarehe 17 mwezi Juni alibadilisha nepi ya mtoto wake.

D'banj ni nani?

  • Ni mwanamuziki mwenye miaka 38, mfanyabiashara na mwandaaji kipindi cha televisheni
  • Alichaguliwa mwanamuziki bora wa tuzo za MTV Europe mwaka mwaka 2007
  • Alishinda tuzo la mwanamuziki bora Afrika mwaka 2014
  • Wimbo wake wa Oliver Twist ulimpa umaarufu wa kimataifa

Mada zinazohusiana