Congo na Somalia ni miongoni mwa nchi kumi hatari kwa wanawake

India imeelezwa kuwa ni hatari kwa maisha ya wanawake

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

India imeelezwa kuwa ni hatari kwa maisha ya wanawake

India imetajwa kuwa ni nchi hatari zaidi duniani kwa usalama wa wanake, kutokana na matukio ya unyanyasaji wa kingono na kushurutishwa kuingia kwenye kazi za utumwa, kwa mujibu wa taasisi ya Reuters.

Afghanistan na Syria zimeorodheshwa kuwa za pili na tatu, katika utafiti uliofanywa na mfuko wa Thomas Reuters uliohusisha wataalamu 550 wa masuala ya wanawake, nchi nyingine zinazofuatia ni Somalia na Saudi Arabia.

Huu ni utafiti uliorudiwa baada ya kufanyika mwaka 2011 ambao ulibaini nchi za Afghanistan, Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo, Pakistan, India na Somalia kuwa ni nchi hatari zaidi kwa wanawake.

Wataalamu wanasema hakuna hatua za kuridhisha zilizofanywa nchini India kuondokana na hatari inayowakabili wanawawake, zaidi ya miaka mitano baada ya kubakwa na kuuawa kwa mwanafunzi ndani ya basi mjini Delhi.

''India imelipa kisogo suala la kuheshimu wanawake, ubakaji, unyanyasaji kijinsia, udhalilishaji wa kingono, vimekuwa vikifanyika bila kukomeshwa'', alieleza Manjunath Gangadhara, afisa katika serikali ya Karnataka .

Data za serikali zinaonyesha kuwa ripoti za uhalifu dhidi ya wanawake zimepanda kwa asilimia 83 kati ya mwaka 2007 na 2016, ambapo kulikuwa na kesi nne za ubakaji zilizokuwa zikiripotiwa kila baada ya saa moja.

Maelezo ya video,

Wanawake wajifunza kutumia teknolojia Kenya

CONGO

Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo ni ya saba kwenye orodha huku Umoja wa mataifa ukitoa tahadhari kwa mamilioni ya watu wanaishi kwenye mazingira ''mabaya sana'' baada ya miaka kadhaa ya umwagaji damu na kutoheshimu sheria.

Utafiti uliofanywa na wanasayansi kutoka nchini Marekani ulibaini kuwa wastani wa wanawake na wasichana 48 hubakwa kila saa nchini humo.

Utafiti, uliochapishwa kwenye jarida la Afya nchini Markeni, umesema kuwa wanawake 400,000 wenye umri wa miaka 15-49 walibakwa katika kipindi cha miezi kumi na mbili kati ya mwaka 2006 na 2007.

Chanzo cha picha, Getty Images

Takwimu Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA) limesema idadi ya waathirika wa visa vya ubakaji vilikuwa juu kwa asilimia 28 mwaka 2015 na mwaka 2016 viliongezeka kwa asilimia 84 ongezeko kutoka mwaka 2013.

Ingawa vikosi vya walinda amani vinaonyesha mzozo kupungua kwa asilimia 25 bado watu wanatahadharisha ongezeko la matukio ya ubakaji nchini humo.

SOMALIA

Somalia imeorodheshwa kuwa ya nne, kutokana na kukumbwa na mgogoro tangu mwaka 1991.Imeorodheshwa ya tatu hatari zaidi kwa wanawake hasa kwa upande wa kupata huduma za afya na tamaduni zinazomweka hatarini mwanamke.Pia imekuwa ya tano kwa wanawake kumiliki rasilimali za uchumi.

Chanzo cha picha, HISANI

Maelezo ya picha,

Baadhi ya wanaume wa Somalia wanaona kuwa nchi za magharibi zinaharibu utamaduni wa Somalia

Utafiti uliofanywa na Umoja wa mataifa mwaka 2011 huko somaliland ulihusisha data zilizokusanywa kutoka kwa wanawake wa umri wa miaka 15-45 kuhusu wanachoamini kuhusu, mtazamo wa wanaume kupiga wake zao.

Wanaume wengi wa kisomali wamekuwa wakikataa kuwa hakuna udhalilishaji dhidi ya wanawake kwenye jamii zao.Wamekuwa wakiishutumu jumuia ya kimataifa kuwa imekuwa ikijibunia takwimu za juu na kupeleka lawama kwa wanaume wa kisomali.

Halikadhalika kumekuwa na utamaduni wa ukimya na hofu kuhusu vitendo vya udhalilishaji ambavyo vimefanya visa hivi visiripotiwe au hata kupatiwa ufumbuzi.

NIGERIA

Nigeria imekuwa ya tisa huku makundi ya haki za binaadamu yakinyooshea kidole majeshi ya nchi hiyo kuhusika na vitendo vya utesaji, ubakaji na mauaji ya raia wakati wa vita vya miaka tisa .Nigeria ilitajwa kuwa ya nne hatari sana sambamba na Urusi kwenye usafirishaji wa binaadamu.Iliorodheshwa ya sita kuwa hatari kwa wanawake kutokana na tamaduni za kumkandamiza mwanamke.