Unahitaji usingizi wa kiwango gani? "Usingizi mdogo unaweza pia kufupisha maisha yako"

woman asleep, floating on a forests Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kulala ni suala muhimu

Ni wanasiasa wangapi na wafanyabiashara utawaskia wakijigamba vile wanalala kwa muda mfupi?

Kukosa kulala usingizi wa kutosha husababisha madhara kwa ubongo wetu na miili yetu pia.

Matthew Walker ni professor ya saikolojia huko UC Berkely.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Professor Matthew Walker

Ameandika kitabu kuhusu "Ni kwa nini Tulala" kitabu chenye uwezo wa kubadili na kurefusha maisha yako.

Anaelewa kuwa watu wana mambo mengi ya kufanya maishani lakini kutokana na ushahidi uliopo hakuna sababu yoyote kuhusu ni kwa nini hatufanyi jitihada za kuongeza muda wa kulala.

Wakati tunapigana na baolojia tunapoteza na kulingana na vile tunajua tumepoteza kwa magonjwa.

Ni kwa nini usingizi ni wa maana?

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Usingizi hautaki mzaha

Ikiwa unataka kuishi hadi uzeeni na kuwa na afya nzuri ni lazima ulale masaa mengi iwezekanavyo, ni lazima uwekeze kwa usingizi mzuri.

Kulala ndio mfumo wa afya unaopatikana kwa njia rahisi ambao kila mtu anahitaji.

Manufaa ya kiafya yanayotokana na kulala yalichangia Prof Walker kuwashauri madaktari kuwapa ratiba ya kulala wagonjwa wao.

Lakini ni lazima uwe ni usingizi wa kawaida, kwa kuwa vidonge vya kualala vimehusishwa na saratani na hata vifo.

Kipi hutokea kwa mwili wakati hatulali?

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kila mfumo wa mwili wa binadamu hupata kujiunda upya wakati mtu analala na mfumo huu huathirika sana wakati mtu anakosa kulala.

Magonjwa ambayo huua watu kwenye nchi zinazoendelea yana uhusiano fulani na kukosa kulala yakiwemo ya moyo. uzani wa mwili kupita kiasi, kisukari, msongo wa akili na kujiua.

Kila mfumo wa mwili wa binadamu hupata kujiunda upya wakati mtu analala na mfumo huu huathirika sana wakati mtu anakosa kulala.

Ni masaa mangapi mtu anastahili kulala ili apate kuwa na afya nzuri?

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Unaweza kuwa na furaha ikiwa utapata usingizi wa kutosha

Jibu fupi ni kati ya saa saba na saa tisa.

Mara unapolala chini ya saa saba, mwili wako unaanza kukumbwa na matatizo ya kiafya ikiwemo ukosefu wa kinga ya mwili.

Iwapo utashinda bila kulala kwa saa 20 mwili wako utakuwa katika hali sawa na mtu mlevi.

Moja ya tatizo la kukosa kulala ni kwamba hauwezi kugundua ni athari zipi zinazokupata.

Ni sawa na mlevi aliye kwenye baa, ambaye huchukua funguo za gari na kusema niko sawa.

Mbona tunalala muda mfupi?

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kulala mchana kunaweza kumkosesha mtu usingizi usiku

1. Kukosa kujua

Licha na jamii na wanasayansi kufahamu mengi kuhusu umuhimu wa kulala, hadi sasa imeshindwa kuuhamasisha umma.

Watu wengi hawafahamu kuhusu umuhimu wa kulala kwa hivyo hawatilii maanani.

2. Hali ya maisha

Kwa jumla tunafanya kazi masaa mengi na kutumia muda mwingi kusafiri.

Tunaondoka manyumbani mapema asubuhi na kurudi jioni kabisa lakini hata hivyo hatutaki kuacha familia na maisha yetu ya kawaida

3. Imani

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Unaweza kusema kuwa huyu mtoto anayelala ni mvivu?

Ikiwa utamuambia mtu kuwa unalala masaa tisa atakutazama na kufikiria kuwa wewe ni mvivu.

Kwa hivyo suala la kulala pia huonekana kama tatizo.

Watu hutembea wakijivuna kuhusu jinsi wanalala saa chache.

4. Mazingira

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Taa humnyima mtu usingizi

Mtu uhitaji giza kuweza kutoa homoni ambazo zitasaidia katika kupata usingizi ulio mzuri.

Lakini tatizo kubwa hapa ni kwamba kila mara taa huwa zimewaka.

Mambo yanayoweza kukusaidia kupata usingizi

Image caption Mambo yanayoweza kukusaidia kupata usingizi