Watu 6 wenye u albino kuwania uongozi katika uchaguzi Malawi

Wanaharakati wanasema hatua hiyo itasaidia kupunguza unyanyapaa dhidi ywa watu walio na ulemavu wa ngozi yaani albinism Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wanaharakati wanasema hatua hiyo itasaidia kupunguza unyanyapaa dhidi ywa watu walio na ulemavu wa ngozi yaani albinism

Chama cha watu wenye ulemavu wa ngozi yaani albino Malawi kimetangaza kutoa watu sita watakaogombea uchaguzi wa Urais na wabunge hapo mwakani, Gazeti la The Guardian Uingereza linaripoti.

Hatua hii inatajwa kuwa njia ya kupambana na mauaji ya watu wenye albinism.

Kuzaliwa na albinism inaweza kuwa kama hukumu ya kifo huko Malawi.

Mbali na taarifa ya vifo vya watu 22 wenye albinism katika kipindi cha miaka minne iliyopita, imeripotiwa kuwa watu wengi zaidi wenye albinism wamepotea na inahisiwa kuwa wametekwa na kuuawa.

Malawi ni moja kati ya nchi hatari duniani kwa watu wanao ishi na albinism-yaani ukosefu wa rangi ya asili katika ngozi, nywele na macho. Ambao wanalengwa ili sehemu zao za mwili ziweze kutumika katika shughuli za kichawi na matendo mengine ya ibada.

Kesi za ongezeko la shughuli za ibada zisizo rasmi na uchawi ambazo zinahusiana na kuua watu wenye albinism kwa ajili ya viungo vyao zime ripotiwa Tanzania na Burundi na kupelekea umoja wa mataifa UM kuunda mamlaka maalum ya kuwalinda watu wenye ugonjwa wa kijenetiki.

Haki miliki ya picha SMART FACTORY
Image caption Kumeshuhudiwa visa vingi vya watu wenye albinism kuuawa kwa uchawi katika baadhi ya mataifa Afrika mashariki ikiwemo Tanzania na Burundi

Mnamo 2016, mtaalamu wa Umoja wa mataifa alionya kuwa watu wapatao 10,000 wenye u albino huenda wakapotea iwapo wataendelea kuuawa kwa ajili ya sehemu zao za miili.

Makaburi pia ya walemavu hao hulengwa na wahalifu wanaotaka kuyatoa mifupa ili wayauze.

Overstone Kondowe, Mkurugenzi wa chama cha watu wenye albinism ama zeruzeru Malawi, alisema wagombea wa kisiasa watasaidia katika kubadilisha jinsi watu wenye albinism wanavyo tazamwa katika nchi ya Malawi.

"Tunataka kuonyesha umma kuwa sisi ni zaidi ya ngozi zetu," alisema.

Elizabeth Machinjiri ni mmoja wa wale wenye mipango ya kusimama kama mbunge katika eneo la Blantyre. Mkurugenzi wa hisani, harakati za watu wenye ulemavu, Machinjiri alisema uzoefu wake ilikuwa muhimu.

Huwezi kusikiliza tena
Mashindano ya urembo ya albino kufanyika Kenya

"Nimeona masuala ya ulemavu yanapuuzwa katika nchi hii," alisema. "Katika bunge letu kuna tu moja au watu wawili wenye ulemavu. Tunahitaji kuwakilishwa. Watu wengine hawawezi kuelewa maumivu na mambo magumu ambayo tunayapitia kila siku."

Machinjiri anasema ataomba shule na hospitali ziwekewe mazingira rafiki kwa walemavu.

Haki miliki ya picha Getty Images

"Watu wengi wanachagua Mbunge kwa sababu ni tajiri. Nasema Hapana, kwa sababu pesa hizo ni binafsi na haziwezi kutumika kwa ajili ya miradi ya maendeleo. Mara baada ya kuchaguliwa, nitahakikisha kwamba nawakilisha sauti na matakwa ya watu wanaoishi katika eneo langu na si tu maoni yangu."

Machinjiri alisema kwamba kukomesha utekaji wa watu wanaoishi na albinism nchini itachukua utashi mkubwa wa kisiasa. Anasema si kazi rahisi kuwashawishi watu, na bado anakazi ya kuongeza fedha kugharamia mchakato wa kampeni.

"Tunahitaji dhamira ya kisiasa katika kupambana na hili," alisema, akisisitiza kwamba mashambulizi yanakuwa zaidi ya kawaida. "Watu wanapaswa kujua kwamba ninasimama kwa sababu. Mimi si mtu wa kuficha uovu kwa kuwa mimi ni mtu jasiri."

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii