Babake Michael Jackson, Joe Jackson aaga dunia

Joe Jackson, alikuwa amelazwa hospitalini kutokana na kuugua saratani Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Joe Jackson, alikuwa amelazwa hospitalini kutokana na kuugua saratani

Baba wa wanamuziki nguli duniani Janet na Michael Jackson ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 89, familia yake imesema.

Jackson amefariki mapema jumatano asubuhi. Na alikuwa amelazwa hospitali kwa maradhi ya saratani ya kongosho, kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari.

Kifo chake kimetokea siku mbili baada ya maadhimisho ya kifo cha mwanaye Michael Jackson aliyefariki miaka tisa iliyopita.

Baba huyo wa familia amechukua nafasi kubwa katika kukuza The Jackson 5, kama vile Michael na Janet Jackson.

Kifo chake kili thibitishwa katika mitandao ya kijamii na baadhi ya watu wa familia yake, ikiwa ni pamoja na binti yakeLa Toya Jackson na wajukuu Taj na Randy Jackson.

Ikumbukwe kuwa watoto wa tano wa Joe Jackson-Jackie, Tito, Jermaine, Marlon na Michael -hawa ndio walio unda kundi la Jackson 5, na baadaye alijiunga mdogo wao wa kiume Randy, ambapo baada ya muda alianza kufanya kazi zake mwenyewe.

Image caption Kundi la The Jackson 5

Mabinti wake watatu - LaToya, Rebbie, na dada yao maarufu zaidi, Janet - wote walifanya muziki wao wenyewe chini ya usimamizi wa Jackson na walipata viwango tofauti vya utambuzi.

Joe Jackson alikuwa mbunifu wa mafanikio ya awali ya watoto wake, lakini baadhi yao baadaye walisema aliwasukuma kwa ari sana mpaka kupelekea unyanyasaji, huku Michael na wengine wakidai kufanyiwa uonevu, unyanyasaji wa kimwili na kuadhibiwa katika ratiba ya kazi.

Baadaye Jackson alikiri kwamba alikuwa akimchapa Michael, lakini alikanusha tukio hilo kujumuishwa kama kupigwa. " Nili mchapa kwa mkanda, lakini sijawahi kumpiga. Unaweza kumpiga mtu kwa fimbo"alimwambia Louis Theroux wa BBC mwaka 2003.

Mahojiano hayo yaligonga vichwa vya habari baada ya Jackson kujibu swali kuhusu Michael, "hatuamini katika mashoga. Siwezi kuwavumilia. "

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kifo chake Joe kimetokea siku mbili baada ya maadhimisho ya kifo cha Michael Jackson aliyefariki miaka tisa iliyopita.

Familia ya Jackson pia ilikua maarufu kutokana na mizozo ya ndani, ambapo mara nyingi ilikuwa wazi mbele ya jicho la uma juu ya hoja mbali mbali lakini pia ugomvi wa fedha na suluhu ilitafutwa kupitia mahakama.

Akizungumza na Daily Mail kabla baba yake hajafariki siku ya Jumatano, Jermaine Jackson alisema baadhi ya wana familia hawakuweza kupata nafasi ya kumuona Jackson katika siku zake za mwisho.

"Hakuna aliyekuwa anajua kile kinachoendelea - Hatukupaswa kuomba, kusihi, na kulazimisha kumuona baba yetu wenyewe, hasa wakati kama huu, "

"Tumekuwa tukiumia sasa. Hatukuambiwa yupo wapi na hatukuweza kupata picha kamili. "

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Joe Jackson

Maisha ya Joe Jackson

Jackson alizaliwa Fountaine Hill, Arkansas mwaka 1928 na ndio mkubwa kati ya watoto watano.

Alisema baba yake alikuwa Profesa wa chuo kikuu, na alikua mtu mwenye msimamo mkali.

Jackson alikuwa na matarajio ya kuwa bondia na baadaye alikuwa mpiga gitaa katika bendi ya mziki laini wa blues, The Falcons, lakini alishindwa kupata mkataba wa kurekodi muziki.

Mwaka 1949 alimuoa Katherine Scruse, ambaye walisoma naye darasa moja kutoka shule ya sekondari ya Washington huko Mashariki mwa Chicago, Indiana. Walikuza watoto wao wakati Jackson akifanya kazi katika kiwanda cha ndani cha chuma.

Mwaka 1957 walipoteza mtoto wao Brandon wakati anazaliwa. Ambaye angelikuwa ni pacha wa Marlon.

Wakati wa miaka ya 1960, Jackson alichukua udhibiti wa kusimamia juhudi za muziki kwa watoto wake wa kiume, ambapo ndipo lilipo zaliwa kundi la The Jackson 5, baadaye wakaingia mkataba na rekodi ya Motown mwaka 1967.

Haki miliki ya picha Getty Images

Jackson 5 iliyumba baada ya Michael kuanza kufanya muziki wake pekeyake na alijitenga na usimamizi wa baba yake.

Jackson sasa alilenga kumsimamia binti yake Janet, ambaye aliendelea na kuwa mwanamuziki nyota na mkubwa.

Taarifa zinasema Jackson katika miongo kadhaa aliendeleza mahusiano ya kimapenzi nje ya ndoa na sekretari wake aliyemzidi miaka 20. Na baadae akazaa nae mtoto wa kike, JohVonnie, mwenye miaka 32 sasa, ambaye pia ni mtoto wa 11 kwa Jackson. Hata hivyo Jackson alibaki katika ndoa yake na Katherine.

Amekuwa katika ndoa na Katherine ambaye anamiaka 88 na kwa pamoja wamezaa watoto tisa kati ya 11 wa Jackson.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii