Je una wasiwasi kuhusu samaki wa Tilapia unayekula?

Tahadhari kuhusu ugonjwa unaoathiri tilapia
Image caption Tahadhari kuhusu ugonjwa unaoathiri tilapia

Ghana imepiga marufuku samaki wote wa tilapia wanaoingizwa chini humo kufuatia kuzuka kwa virusi ambavyo ni hatari kwa sekta yote ya tilapia kote duniani.

Virusi hivyo vinayojulikana kama Tilapia Lake Virus (TilV) havina tiba na vimepatikana kwenye mashamba ya tilapia barani Afrika, Asia na Amerika Kusini.

Wizara ya uvuvi nchini humo ilisema kuwa Marufuku hiyo ya miezi sita itaanza kutekelezwa siku ya Jumapili na itaathiri samaki walio hai na hata wale wamekufa.

Viwango vya samaki nchini Ghana vimekuwa vikishuka kutokana na uvuvi ulio haramu.

Kuna mashamba machache ya tilapia nchini Ghana na yanafanyika kwa kiwango kidogo.

Je virusi vya TilV vina madhara gani kwa binaadamu?

Kwa mujibu wa shirika la chakula duniani FAO, virusi hivyo havina madhara kwa afya ya umma lakini kufariki kwa samaki kutokana na virusi hivyo kunazusha maswali na wasiwasi kuhusu usalama wa chakula na lishe bora.

Tayari bei ya samaki hao imekuwa ikibadilika kutokana na uhaba unaoshuhudiwa katika baadhi ya maeneo na pia kwa kutambuliwa virutubishi vyake vinavyofanya aina hiyo ya samaki kuwa muhimu hususan katika nchi zinazoendelea kwa walaji wake wengi.

Mwaka uliopita shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) lilitoa tahadhari kuhusu virusi hatari vilivyokuwa vikiathiri samaki aina ya tilapia

FAO ilizitaka nchi zilizokuwa zikiagiza samaki wa tilapia kuchukua tahadhari zaidi.

Wakati huo virusi hivyo viliripotiwa kuathiri nchi za Colombia, Equador, Misri, Israel na Thailand.

Umuhimu wa tilapia

Tilapia ndiye samaki wa pili muhimu sana duniani kwa chakula, ajira kwa mapato ya nyumbani na kwa kuuza nje na kuwapa kipato mamilioni ya watu wakiwemo wakulima na wafanyabiashara wadogo.

Bei yake nafuu, ustahilivu wao kwa kilimo na kutopata magonjwa kwa urahisi huwafanya tilapia kuwa muhimu wa protini hasa kwa nchi zinazoendelea na kwa watu maksini kwa mujibu wa FAO.

Mwaka 2015 uzalishaji wa tilapia dunia nzima ulifika tani 6.4 wa thamani ya takriban dola bilioni 9.8 ukichangia biashara ya dola bilioni 1.8 kote duniani.

Matumizi ya tilapia

Uganda

Moja wa wazalishaji wakubwa wa tilapia Afrika kutokana na kilimo na pia kutokana na uvuvi wa kawaida.

Wana kiwango kikubwa cha tilapia wanaotokana na kilimo lakini wanapungua. Baadhi yao huuzwa nje hasa kwenda kwa Muungano wa Ulaya.

Matumizi yanakadiriwa kuwa ya kiwango cha 13.6 na tilapia ni chakula cha kitamaduni nchini Uganda.

Nchi hii ya Afrika Mashariki inapakana na nchi ambazo watu wanakula samaki kwa wingi zikiwemo DRC, Sudan Kusini, Kenya. Tanzania na Rwanda.

Kenya

Moja wa wazalishaji wakuu wa talapia inayotokana na kilimo barani Afrika.

Tilapia ni chakula muhimu nchini Kenya. Lakini nchi hiyo inakadiriwa kukumbwa na upungufu wa metriki tani 10,000 za tilapia.

Kiwango ambacho maduka ya jumla yanaagiza kinaongezeka.

DRC

Mahitaji ya samaki ni ya juu kuliko uzalishaji wake. Samaki huchangia asilimia 25 hadi 50 ya protini nchini humo.

Kilimo cha samaki ni cha chini sana. Nchi hiyo inatagemea uagizaji wa samaki hasa kutoka nchi zingine na pia kutoka China.

Ina watu wengi takriban milioni 70. Tilapia ni chakula muhimu nchini DRC. Nchi hii inakumbwa na uhaba wa tilapia wa karibu metriki tani 30,000.

Kuna ushidani kutoka kwa bidhaa za samaki zilizokaushwa. Bei ni nzuri, kilo moja ya tilapia inaweza kuuzwa kwa dola tano.

Mada zinazohusiana