Diamond Platinumz: Daylan ni mwanangu halisi 'msiniletee'

Diamond Haki miliki ya picha AFP/Getty

Msanii wa Tanzania Diamond Platnumz amewapuuzilia mbali wanaodhania kwamba yeye sio baba wa kweli wa mtoto wake wa kiume wa mwanamitindo Hamisa Mobetto.

Diamond alichapisha ujumbe mkali katika mtandao wake wa Instagram akithibitisha kuwa Daylan ni mwanawe anayempenda sana.

Hatua hiyo inajiri baada mwanamuzilki huyo kuchapisha kanda fupi ya video akivumisha ziara yake ya Marekani.

Kanda hiyo fupi ya video inamuonyesha Diamond akizungumza kuhusu kazi yake na familia.

Anazungumzia vile atakavyokuwa mbali na familia yake kwa takriban mwezi mmoja suala litakalomfanya kutowaona dada zake, mamake na watoto wake.

Kanda hiyo ya video hatahivyo iliwaonyesha wanawe wawili aliyozaa na mfanyibiashara wa Uganda Zari Hassan.

Video hiyo haikumuonyesha mwana wa Hamissa Mobetto, hatua iliowakera mashabiki wake waliotoa hisia tofauti kabla ya Diamond kuchapisha ujumbe huu.

''Huyu ni mwanangu... na ataendelea kuwa mwanangu maisha yangu yote, tena kipenzi changu... .Hakuweza kuwepo kwenye clip iliyopita sababu @lukambaofficial Hakuwa na clip ya mimi na yeye ya Hivi karibuni... na si Vinginevyo... ... .Halaf cha kuongeza, msiniletee Uteam wenu kwa Watoto zangu! Wote ni watoto wangu, Nawapenda na siwezi mtenga wala kumbagua yoyote... ..👍🏼 @deedaylan 💖🤴💖

Haki miliki ya picha Diamond/Instagram

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii