Wafungwa Kenya wafunzwa yoga kuwapunguzia mawazo
Huwezi kusikiliza tena

Wafungwa Kenya wafunzwa yoga kuwapunguzia mawazo

Je umeshawahi kufikiria jinsi watu walioko magerezani wanavyoishi siku baada ya siku bila uhuru wa kufanya lolote na mahangaiko tele ya mawazo kuhusu maisha yao na jamii walizoziacha nyumbani?

Wanahabari wa BBC Anythony Irungu na Anne Ngugi walizuru gereza la wanawake la Machakos na kushuhudia wafungwa wakifanyishwa mazoezi kupitia wa mazoezi ya maungo, kutafakari na kudhibiti pumzi maarufu kama yoga.

Mazoezi hayo huwasaidia wafungwa kusukuma siku gerezani na angalau wapate lepe la usingizi.