Hii ndio sababu kwanini ni muhimu kumuona daktari mmoja kila unapokuwa mgonjwa.

daktari amuhudumia mgonjwa

Je umebadilisha mara ngapi madakatari unaowaona kila unapokuwa mgonjwa? Huenda unahitaji kubadili mwenendo huo sasa maana utafiti mpya umebaini kuwa watu wanaomuona daktari mmoja kila wanapokuwa wagonjwa wanapunguza viwango vya vifo.

Utafiti umebaini kuwa kuna faida kubwa ya kuwaona madakati jumla na hata wataalamu na hilo limeshuhudiwa katika tamaduni na mifumo tofuati ya afya.

Wataalamu kutoka chuo kikuu cha Exeter wamesema suala kuu katika utoaji wa matibabu ni "kuokoa maisha ya watu" lakini hilo limesahahulika.

Madaktari wengi wanasema wanatambua thamani ya mgonjwa kutaka kumuona 'daktari wako binafasi'.

Hatahivyo kutokana na shinikizo la kazi , wagonjwa hulazimika kusubiri kwa muda mrefu zaidi kumuona dakatari wao binafsi .

Ni jambo lenye manufaa makubwa wakati mgonjwa anaonekana kwa muda mrefu na dakatari mmoja hususan kwa wale walio na magonjwa makubwa na ya muda mrefu mfano matatizo ya akila moyo na kadhalika yanayohitaji kushughulikiwa kwa uzito zaidi.

Daktari anakuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kumtibu mgonjwa kutokana na kuwana ufahamu wa historia ya ugonjwa anaougua.

Utafiti uliochapishwa katika jarida la BMJ Open, ulihusisha ukaguzi wa jumla ya wagonjwa 22 kutoka mataifa 9 yakiwemo England, Ufaransa, Marekani Canada na Korea kusini.

Kulishuhudiwa visa kidogo vya vifo katika matokeo ya utafiti wa wagonjwa 18 waliotibiwa na daktari huyo huyo kwa kipindi cha miaka 2 ikilinganishwa na wagonjwa wengine.

Watafiti wanasema ni muhimu kuendeleza matibabu kwa daktari mmoja na ni suala linalostahili kutiliwa mkazo katika kupanga utoaji huduma za afya.

Haki miliki ya picha Getty Images

Hilo litawezekana vipi?

Prof Philip Evans, kutoka chuo kikuu cha Exeter anasema: "muendelezo wa huduma za afya huwezekana wakati mgonjwa anapata kuonana na daktari mara kwa mara na kupata kujuana.

"Hili huchangia mawasiliano mazuri zaidi , mgonjwa huridhika, na huchangia mgonjwa kufuata vyema maagizo ya daktari wake na pia linaweza kupunguza idadi ya wagonjwa katika hospitali."

Watafiti wanasema "Kwa muda mrefu wagonjwa wanatambua ni muhimu kujua aina ya daktari wanayekwenda kumuona na iwapo wanaweza kweli kuwasiliana vizuri na kuwahudumia vyema.

Ni wazi sasa kwamba kiwango cha matibabu ni muhimu lakini zaidi ni suala la 'kuokoa maisha zaidi'.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii