Kombe la Dunia 2018: Furaha na Huzuni katika michuano hiyo kufikia sasa

Kiungo wa Japan Hotaru Yamaguchi (K) na wenzake washerekea kufuzu kwao hatua ya mchujo Kombe la Dunia Urusi 2018. Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mienendo maridadi ya Japan imetuzwa. Imejikatia tiketi ya kushiriki hatua ya raundi ya pili Kombe la Dunia kulingana na sheria za 'fair play'

Habari zisizopendeza kwa wapenzi wa soka - zaidi ya thuluthi mbili ya mechi za Kombe la Dunia FIFA 2018 Urusi zimechezwa, yaani (Mechi 48 kati ya 64).

Kwa upande mwingine, habari nzuri ni kuwa zilizosalia sasa, sio tu muhimu bali huenda pia ndizo ambazo hazitasahaulika kwani miujiza, historia na mishangao ya ngarambe za Kombe la Dunia itashuhudiwa tena.

Lakini kufikia sasa, ni yapi ya kuzungumziwa yaani ''yaliyovutia'' kufikia awamu hii ya kwanza ya dimba hili?

Japanese “tabia nzurihulipa

Dimba la Dunia 2018 ilianzisha kadi za njano kama kigezo cha kuamua nani atakayefuzu iwapo timu zitakuwa zimetoshana kwenye vigezo vingine vyote uwanjani.

Hilo liliiwezesha Japan kuipiku Senegal Kundi H na kutuzwa nafasi timu 16 bora za mwisho.

''The Blue Samurai'' wa Japan walifungua Kombe kwa kuikung'uta Colombia, kutoka sara 2-2 na Senegal, lakini ilipoteza mechi ya mwisho ya makundi dhidi ya Poland (1-0) na kutishia kuinyima bara Asia timu kwenye hatua ya mchujo Urusi 2018.

Lakini ni Japan ipi itajitokeza dhidi ya washindi wapendekezwa Ubelgiji siku ya Jumapili?

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Croatia ni kati ya timu tatu zilizoshinda mechi zake zote za makundi.

Uruguay, Ubelgiji na Croatia wavuma

Ni timu tatu pekee zilisajili rekodi za kuvutia hatua ya makundi na kuwatia uoga wapinzani watakaocheza nao hatua ijayo.

Ikiongozwa na nyota wake wanaosakata ligi kuu ya soka Uingereza, Ubelgiji imekuwa timu yenye mabao zaidi Urusi hadi sasa (mabao tisa) na kuthibitisha kupigiwa upatu kufanikiwa na kufika mbali dimbani.

Wakishinda Kombe hili, watawapokonya Uruguay taji la kuwa taifa dogo kuwahi kuinua Kombe la Dunia, lakini Luisito Suarez na wenzake ni wawaniaji hatari baada ya kulikunja jamvi la Kundi A na ushindi wa 3-0 dhidi ya wenyeji Urusi.

Kwa Croatia, wamezua mjadala baada ya kumaliza kileleni Kundi A mbele ya Argentina, Nigeria na Iceland.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Brazil ni moja kati ya wawakilishi wanne wa Amerika ya Kusini waliosalia Urusi

Mawimbi ya Amerika ya Kusini

Wawakilishi wanne kati ya watano wa Amerika ya Kusini wameponea kutolewa hatua za makundi.

Brazil, Colombia, Argentina na Uruguay huenda pia wakachukua nusu ya nafasi za robo fainali kwani hakuna uwezekano wa kukutana kwao.

Diamond ajitetea kuhusu mwanawe Daylan

Ni ujumbe kutoka kwao hadi FIFA katika kipindi ambacho shirikisho hilo linalosimamia soka linajadili upanuzi wa Kombe la Dunia hadi timu 48 na kuzidisha nafasi kwa bara tofauti.

Peru, mbali na kutofuzu hatua za makundi imemaliza nafasi nzuri kushinda Australia Kundi C.

Peru wamekuwa nje ya Kombe hili tangu 1982, wakati Australia imeshiriki makala matatu yaliyopita kwa mfululizo.

Image caption Russia 2018 imeshuhudia mabao 122 mechi 48

Hadi kwenye wavu

Kulingana na FIFA, magoli 122 yametiwa kimiani katika mechi 48 za hatua za makundi, kumaanisha mabao 2.54 yamefungwa kila mechi.

Yaani, Kombe la Dunia Urusi 2018 ndilo Kombe la pili kuandikisha mabao mengi karne ya 21.

Mashabiki wanahisi kuwa hatua ya mchujo na kumakinika kwa timu hazitapelekea mabao machache.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Serbia ndio timu iliyo na pumzi zaidi hatua za makundi

Warusi waachwa

Baada ya kutia kapuni ushindi maridadi uliowapunga mashabiki wa nyumbani, timu ya Urusi ilianza kulengwa kwa madai baada ya kufichuliwa kuwa ndio walikimbia masafa marefu zaidi ya washiriki wengine wote uwanjani Kombe la Dunia.

Sakata za hivi karibuni za matumizi ya dawa zilizokatazwa kwenye spoti zinazihusu wasimamizi wa mashirika ya spoti ya taifa hilo, zilianza kujitokeza.

Lakini mwisho wa hatua ya makundi, Urusi iliachwa nyuma.

Chemsha bongo: Mara ya kwanza Ujerumani kubanduliwa katika raundi ya kwanza katika michuano ya Kombe la Dunia ilikuwa mwaka gani?

Serbia inaongoza kwa kukimbia kilomita 339, mbele ya mabingwa wa 2014 Ujerumani waliokimbia kilomita 335.59.

Kwaheri, Afrika

Kwa mara ya kwanza tangu 1982, Afrika haitawakilishwa hatua ya mchujo katika Kombe la Dunia.

Senegal, Nigeria, Morocco, Tunisia na Misri watafuatilia michuano iliyosalia ya Kombe la Dunia kwenye runinga.

Wanoumia zaidi na wenye uchungu ni mashabiki wa Senegal, kwani timu yao ni ya kwanza kuondoka kutokana na masuala ya kinidhamu.

Kwa hakika sasa ni muda wa wakuu wa soka Afrika kutathmini ni wapi bara lilikosea ngarambe hizo za dunia.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mabingwa Ujerumani walizalisha nafasi nzuri za kutikisa wavu lakini hawakuweza kubandika mikwaju yao kambani.

Uzembe wa Ujerumani

Huenda tukaliangalia kwa jicho la nuksi ya kuwa bingwa mtetezi tunapolizungumzia Ujerumani kwani ndio mabingwa wa nne kati ya mabingwa watano kutolewa hatua ya makundi karne hii ya 21.

Mbali na kukosa kujaza mapengo yaliyoachwa na mastaa waliostaafu kama Philipp Lahm, Bastian Schweinsteiger na Per Mertesacker, Wajerumani walizembea mbele ya goli.

Takwimu za FIFA zinaonyesha kuwa Ujerumani ndio timu yenye majaribio mengi langoni kati ya timu 32 zote dimbani. Ilibuni nafasi (75), lakini imefunga mabao matatu tu - ikifungwa manne.

Ni kinaya kuwa Urusi, timu iliyosajili nafasi chache za kufunga mabao, iliyapachika wavuni mabao 8 kati ya nafasi 18 ilizobuni.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Licha ya kutemwa katika mashindano, kumbukumbu imesalia ya madhambi waliotenda Korea kusini

Ukatili wa Korea

Mbali na kuliaga Kombe hili hatua ya makundi, Korea Kusini wameondoka Urusi na ushindi wa kihistoria wa kuwazamisha Ujerumani.

Aidha, wanafunga safari wakiwa na taji jipya la “wanyoaji”.

Korea ndiyo timu iliyosababisha madhambi zaidi uwanjani (63), na kuipiku Morocco yenye makosa (62) na kupelekea mikwaju ya ikabu dhidi yake.

Ziara ya rais Mnangagwa Tanzania ina umuhimu gani?

''Wakarimu'' kati ya timu zote ni jirani wa Korea Kusini, Japan , waliotekeleza makosa 28. Nidhamu yao ya hali ya juu imewafaa kwa kuwawezesha kufuzu kutoka Kundi H.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Uhusiano wa Kiungo wa Uruguay Matias Vecino na Inter Milan itafaa Uruguay?

Kwani Brazil, Croatia au Uruguay wametua fainali tayari?Sheria ya “Inter Milaninasema

Ukiangazia takwimu tatanishi, basi, bingwa ni kati ya watatu hao.

Tangu 1982, kila fainali ya Kombe la Dunia imemshirikisha mchezaji wa klabu ya Inter Milan ya ligi ya Italia .

Kufikia sasa ni wachezaji watatu pekee wa Mababe wa Milan wamesalia Urusi nao ni beki wa Brazilia Miranda, Kiungo wa Uruguay Matias Vecino na winga wa Croatia Ivan Perisic.

Msiseme hatujawaonya!

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mtambo wa VAR ni mojawapo ya masuala yaliyozua gumzo Kombe la Dunia hadi sasa

VAR ndio inawashawishi waamuzi?

Kulingana na jarida la Brazilia Folha de S. Paulo, baada ya kutathmini mechi 40 zilizopigwa nchini Urusi 2018, mtambo wa refa msaidizi wa kiteknolojia, (VAR) ulibadili uamuzi wa refa mara 9 kati ya hali 11 ambapo mwamuzi huyo mkuu aliamua kushauriana na mtambo huo nje ya uwanja.

Sita kati ya maamuzi hayo tisa yaligeuka kuwa penalti ambazo hazikutunukiwa awali.

Waliofuzu 16 bora Kombe la Dunia, na waliotupwa nje

Takwimu zaidi ikiwemo kutoka jarida la Uingereza la The Times,- VAR ilikosea kipindi kimoja tu kati ya vipindi 15, kulingana na bodi ya kimataifa inayosimamia utungaji wa sheria za soka, International Board.

Inaamini mkwaju uliopewa Iran ilipotoka sare 1-1 dhidi ya Ureno si sahihi.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii