Ronaldo akataa kuzungumzia hatma yake baada ya Ureno kutimuliwa Kombe la Dunia

Cristiano Ronaldo wins a header against Uruguay

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Ronaldo alifanikiwa kulenga mara moja tu dhidi ya Uruguay

Cristiano Ronaldo amesama huu sio wakati wak kuzungumzia hatma yake ya kimataifa baada ya Ureno kuondalewa Kombe la Dunia.

Kipiga cha mabao 2-1 na Uruguay siku ya Jumamosi kiliwapeleka mabingwa hao wa Ulaya nyumbani.

Kocha wa Ureno Fernando Santos alisema ana matumaini kuwa nahodha wake ambaye atakuwa na umri wa miaka 37 wakati wa kombe la dunia ambalo litafanyika huko Qatar atasalia kuwasaidia wachezaji wadogo kuinuka.

"Timu hii kawaida itapigana kwa nguvu zake zote,"alisema Ronaldo.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Ronaldo baada ya kukosa penalti dhidi ya Iran (kushoto) na baada ya kufunga dhidi ya Morocco (kulia)

Ronaldo alifunga mabao manne, ikiwemo hatitriki dhidi ya Uhispania kuifikisha katika kundi la 16 peke yake lakini hakuweza kuendelea kupita mechi za makundi.

Yeye na mshindani wake wa siku nyingi Lionel Messi sasa wameondoka mashindano ya Kombe la Dunia baada ya Argentina kuelekea nyumbani siku ya Jumamosi kufuatia kushindwa kwa mabao 4-3 na Ufaransa.

Mshambuliji wa Barcelona Messi, 31, pia hajafunga katika awamu ya maondoano ya Kombe la Dunia na anatathmini hatma yake katika soka ya kimataifa.

Lakini kwa sasa Ronaldo hakutaka kuzungumzia hatma yake na Ureno.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kocha wa Ureno (kulia) anataka Ronaldo kuichezea nchi yake wakati wa ligi ya Uefa ambayo itaanza Septemba

"Sio wakati wa kuzungumzia hatma yetu sisi wachezaji na kocha," alisema.

Mimi kama nahodha ninajivunia wachezaji, makocha na watu walihakikisha kuwa kila kitu kimekwenda vyema.

Kushindwa na Uruguay inamaanisha kuwa Ureno ilirudia matokeo ya Afrika Kusini ya mwaka 2010, ambapo iliondolewa kwa kundi la 16, kinyume na matokeo ya Ujerumani mwaka 2006 ilipomaliza namba nne na namba tatu katika kombe la mwaka 1966 huko England.

"Ningependa kuwapongeza Uruguay, ambao walifunga mara mbili, lakini pia ningependa kuwapongeza Ureno kwa kile walikifaya," aliongeza Ronaldo.