Je ni kwanini serikali ya Uganda inatoza kodi ya mitandao ya kijamii OTT?

Raia Uganda wametakiwa kulipa kodi ili kuweza kutumia mitandao ya Whatsapp, Facebook, Twitter na mengineyo ya kijamii

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Raia Uganda wametakiwa kulipa kodi ili kuweza kutumia mitandao ya Whatsapp, Facebook, Twitter na mengineyo ya kijamii

Watumiaji mitandao ya kijamii Uganda hawana mahala pa kujificha kukwepa tozo la kodi ya mitandao ya kijamii iliyoidhinishwa na serikali.

Agizo jipya limetolewa kwa makampuni ya mawasiliano Uganda kuzuia mfumo unaoruhusu watumiaji mitandao kuweza kuingia katika mitandao hiyo -VPN - ambao baadhi ya wateja sasa wanaitumia kuvuka vizuizi vilivyowekwa kuwaruhusu kuingia katika mitandao hiyo ya kijamii na kukwepa kulipa Kodi.

Sasa serikali imesema hilo linaelekea kwisha. Wanachi watakuwa hawana njia ya kukwepa kulipa kodi ya mtandao.

Serikali inasema hatua hiyo itasaidia kuingiza kipato kinachohitajika pakubwa, lkini wanaharakati wanaikosoa hatua hiyo kuwa ya jaribio la 'kubana' uhuru wa kuzungumza.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka gazeti la wiki, Weekly Observer, mkurugenzi mtendaji wa tume ya mawasialiano Uganda, Godfrey Mutabazi, kampuni za simu zitaanza kuzuia taratibu programu tumishi za mfumo wa VPN unaowasaidia Waganda kukwepa kulipa kodi ya mitandao ya kijamii.

Ni kwanini serikali inatoza kodi hii ?

Rais Yoweri Museveni alishinikiza mageuzi hayo , akieleza kuwa mitandao ya kijamii huchangia kuenea kwa udaku nchini, anaoutaja kuwa maoni, upendeleo, matusi na hata chati kwa marafiki.

Katika barua aliyomuandikia waziri wa fedha mnamo Machi, rais Museveni amesema kodi kwa mitandao ya kijamii inaweza kuongeza kipato cha serikali, na kupunguza mikopo inayochukua serikali na pesa za ufadhili.

Ameongeza kwamba haungi mkono kodi iitozwe kwa matumizi jumla ya mtandao kwasababu hili litaathiri matumizi yake kwa misingi ya 'elimu, na utafiti '.

Waziri wa habari na mawasiliano Uganda Frank Tumwebaze pia ametetea kuidhinishwa kwa kodi hiyo, akisema kwamba fedha zitakazopatikana zitatumiwa 'kuwekeza katika rasilmali zaidi za kimitandao'.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Rais Yoweri Museveni anasema mitandao ya kijamii huchangia kuenea kwa udaku nchini.

Agizo hilo la kulipa kodi kwa mitandao kama Whatsapp, Facebook, Twitter na kadhalika, limeanza kufanya kazi tarahe mosi Julai nchini.

Agizo jipya limepokewaje ?

Kumeibuka hisia mchanganyiko miongoni mwa raia Uganda wengi wakieleza walivyoathirika nalo, huku wengine kwa shingo upande wakilipa kodi hiyo.

Hii ni mifano ya waliofanikiwa kuingia katika mitandao ya kijamii ambao walitumia fursa kuelezea hisia zao kuhusu agizo hilo jipya.

Wengine walitumia fursa kufanya stizai kuhusu anayoona yaliomuhimu kushughulikiwa kuliko maamuzi ya kutoza kodi .

Amemithilisha hatua ya Uganda na tangazo la hivi juzi Rwanda kuunda gari lake la kwanza nchini

Kuna na walio fanikiwa kuilipa kodi hiyo kama huyu katika ujumbe wake huu kwenye Twitter amekiri kulipa ila anaulizani wangapi wengien walio na uwezo wa kulipa kiwango kinachotozwa cha kodi ya mtandao?

Inakadiriwa kwamba zaidi ya asilimia 70 ya raia nchini Uganda wana simu za mkononi.

Ni 41% ya raia nchini wanatumia mtandao Uganda kufikia mitandao ya kijamii kama Facebook na Twitter iliyo maarufu zaidi nchini humo.

Hatahivyo kuna walio tilia shaka uwezo wa kuendeleza kutekeleza kwa urahisi agizo hilo kutokana na kwamba baadhi bado hawajaelewa wazi ni vipi maafisa wa serikali wataweza kuwatambua wale watakaokwepa vizuizi vya serikali na kuingia katika mitandao ya kijamii.

Mataifa mengine Afrika mashariki katika siku za hivi karibuni yamepitisha sheria za kudhibiti matumizi ya mitandao ambazo wakosoaji wanasema zinaathiri uhuru wa kujieleza.