Kenya miongoni mwa maeneo mapya ya kihistoria yaliotangazwa na UNESCO duniani

Makazi kavu: Kenya

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Kiingilio cha ukuta wa Thimlich Ohinga Kenya

Shirika la utamaduni la Umoja wa Mataifa, UNESCO limetangaza maeneo mapya ya kihistoria duniani kote.

Kuorodheshwa katika orodha hiyo kuna yapa maeneo hayo ulinzi wa kisheria chini ya mikataba ya kimataifa, UNESCO imesema.

Shirika la utamaduni la Umoja wa Mataifa, lililo fanya mkutano huko Bahrain, wamekubaliana ni maeneo gani duniani ambayo kwa ajili ya historia ya ulimwengu yanahitaji hifadhi kwa ajili ya umuhimu wao wa kitamaduni, kihistoria au kisayansi.

Makazi kavu: Kenya

Thimlich Ohinga ni ukuta mkubwa zaidi wa makazi ulio jengwa kwa mawe katika kanda ya ziwa Victoria Kenya.

Makazi hayo yapo kaskazini magharibi mwa mji wa Migori, inaaminika kwamba umejengwa katika karne ya 16 na inaonekana kuwa ulihudumu kama ngome ya jamii na mifugo.

Unesco unautaja kama mfano pekee wa desturi ya jamii ya kichungaji wa kwanza katika kingo za ziwa Victoria".

Mji wa Bandari ya Kale: Qalhat, Oman

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Mji wa Bandari ya Kale: Qalhat, Oman

Katika Mashariki ya Omani, mji wa Qalhat ilikuwa ni bandari kubwa katika karne ya 11 na 15. Hii ni shuhuda kubwa ya akiolojia kwani ndio kiungo kati ya mashariki mwa Saud Arabia na Dunia kwa ujumla.

Maeneo ya Wakristu yaliyo fichwa: Nagasaki, Japan

Chanzo cha picha, AFP

Eneo hili katika kisiwa cha Kyushu lina vijiji 10, kuna ngome na kanisa kuu na yali jengwa katika karne ya 18 na 19, wakati ambapo imani ya Kikristo ilipigwa marufuku nchini Japan.

Hii inaashiria shughuli za mwanzo za wamisionari wa Kikristo na walowezi katika nchi ya Japan, na inabeba ushuhuda wa kipekee kwa utamaduni ulio kuzwa na wakristu walio jificha", Unesco inasema.

Usanifu wa Majengo: Mumbai, India

Chanzo cha picha, AFP

Tangu imekuwa kitovu cha biashara ya kimataifa mwishoni mwa karne ya 19, Mumbai ili jiingiza katika mradi wa mpango miji, kujenga majengo mazuri kwa matumizi ya makazi na biashara.

Majengo ya Victoria ni majengo ya kisasa zaidi yamewekewa veranda na maeneo mazuri ya kupumzika, wakati majengo ya Art Deco ni majengo ya sinema, ghorofa na hospitali yaliyo pangwa katika safu ya rangi.

"Majengo haya mawili ni shuhua ya awamu ya kisasa ambayo Mumbai imepitia katika kipindi cha karne ya 19 na 20," UNESCO linasema.

Bonde la Al-Ahsa: Saudi Arabia

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Bonde la Al-Ahsa: Saudi Arabia

Al-Ahsa, katika Rasi ya Uarabuni Mashariki, ni bonde kubwa zaidi duniani na limekuwa nyumbani kwa binadamu kutoka zama za Waneolithiki hadi sasa.

Pia katika eneo hili kuna miti ya minazi milioni 2.5, bustani, mifereji, chemchemi, visima, ziwa lililo kauka, mifereji ya maji, majengo ya kihistoria na maeneo ya akiolojia.

UNESCO inapatazama hapa kama mfano pekee wa mahusiano ya binadamu na mazingira"

Milima ya Ibada: Korea ya Kusini

Chanzo cha picha, AFP

Milima Sansa iliyopo eneo la kusini mwa Korea Kusini imekuwa ukiendeshwa kama vituo vya imani tangu karne ya 7. Mahekalu hayo saba yana viwanja vya wazi na kumbi za mihadhara.

UNESCO inayaita maeneo haya kuwa ni maeneo matakatifu ambayo yame himili kuwepo kama kituo cha ibada na sehemu ya kila siku katika maisha ya kidini mpaka sasa.

Mazingira ya akiolojia Sassanid : Iran

Chanzo cha picha, EPA

Mchanganyiko wa miundo iliyoimarishwa, majumba na mipango miji- katika maeneo nane ya akiolojia katika jimbo la Fars - kurudi nyuma enzi za himaya Sassanian, kutoka karne ya 3 na 5.

Eneo hili sio tu lina akisi mpangilio bora wa asili wa majengo lakini pia lina shuhudia ushawishi wa sanaa ya Kirumi na mila za tamaduni ya Waparthi, Unesco linasema.