Ni kwanini jina la Patrice Lumumba Ubelgiji, limezusha hasira DRC
Huwezi kusikiliza tena

Kwanini jina la Patrice Lumumba Ubelgiji, limezusha hasira DRC

Ubelgiji imelipa bustani moja katika mji mkuu Brussels jina la mpiganiaji uhuru wa DRC, marehemu Patrice Emery Lumumba kama njia ya kumkumbuka na kumuenzi shujaa huyo.

Lumumba aliuawa mnamo 1961, mwaka mmoja tu baada ya kudai uhuru wa nchi hiyo kutoka kwa wakoloni Ubelgiji.

Wataalamu wanasema hatua hiyo ni ishara ya dhahiri ya Ubelgiji kuiomba radhi Congo kwa kuhusika katika mauji ya muasisi huyo wa DRC.

Lakini sio raia wote wa Congo wanaoifurahia hatua hiyo.

Phillipe Unji Yangya ni waziri wa zamani wa maendeleo DRC amezungumza na Mbelechi Msochi wa BBC Swahili:

Mada zinazohusiana