Kwa Picha: Magufuli akutana na marais wa zamani, na Edward Lowassa

Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli amekutana na marais wa zamani pamoja na viongozi wengine wa zamani walioshikilia nyadhifa mbalimbali serikali.

Rais huyo aliwapa mwaliko wa kukutana naye ikulu, ambapo mkutano ulifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam.

Picha zilizotolewa na ikulu hata hivyo zinaonesha Bw Kikwete hakuhudhuria mkutano huo.

Haki miliki ya picha IKULU

Hii ni mara ya kwanza kwa Rais Magufuli kukutana na viongozi hao wakuu wastaafu na taarifa ya ikulu imesema lengo lilikuwa "kupokea ushauri na maoni yao juu ya uendeshaji wa Serikali na mustakabali wa Taifa".

Haki miliki ya picha IKULU
Image caption Dkt Magufuli akisalimiana na Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi
Haki miliki ya picha IKULU
Image caption Dkt Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim
Haki miliki ya picha IKULU
Image caption Magufuli akisalimiana na Spika Mstaafu Anne Makinda. Aliyeketi karibu na Bi Makinda ni Spika Msaafu Pius Msekwa
Haki miliki ya picha IKULU
Image caption Dkt Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Fredirick Sumaye
Haki miliki ya picha IKULU
Image caption Dkt Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa David Msuya
Haki miliki ya picha IKULU
Image caption Dkt Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda
Haki miliki ya picha IKULU
Image caption Dkt Magufuli akisalimiana na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt. Amani Abeid Karume kabla ya kikao
Haki miliki ya picha IKULU
Image caption Picha ya pamoja ya viongozi waliohudhuria

Ni miaka miwili na nusu sasa tangu serikali ya Awamu ya Tano yake Rais Magufuli ilipoingia madarakani.

Bw Lowassa aliwania urais mwaka 2015 dhidi ya Dkt Magufuli lakini akamaliza akiwa wa pili.

Miongoni mwa waliofika kulikuwa na rais wa zamani Benjamin Mkapa.

Haki miliki ya picha IKULU
Haki miliki ya picha IKULU
Haki miliki ya picha IKULU
Haki miliki ya picha IKULU
Image caption Waziri Mkuu Mstaafu John Samwel Malecela akizungumza katika mkutano huo Ikulu jijini Dar es Salaam
Haki miliki ya picha IKULU
Haki miliki ya picha IKULU

Rais Magufuli ametumia fursa hiyo pia kuwaeleza viongozi hao juhudi mbalimbali zinazofanywa na Serikali yake ambapo ni pamoja na uongeza ukusanyaji wa mapato ya Serikali ambao amesema umeongezeka kutoka Shilingi Bilioni 800 hadi kufikia Shilingi Trilioni 1.3 kwa mwezi.

Aidha, kuna kuanza ujenzi wa reli ya kisasa kuanzia Dar es Salaam hadi Dodoma utakaogharimu Shilingi Trilioni 7.26, kujenga mradi wa umeme katika mto Rufiji (Stieglers' Gorge) utakaozalisha Megawati 2,100 za umeme, kutoa elimu ya msingi na sekondari bila malipo na kuongeza mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu.

Haki miliki ya picha Ikulu

Unaweza kusoma pia:

Mada zinazohusiana