Baba aliyemnyonyesha mtoto wake mchanga wakati mama hakuweza

Dad breastfeeds newborn daughter Haki miliki ya picha Maxamillian Kendall Neubauer
Image caption Baba amnyonyesha mtoto wake mchanga

Wakati wanandoa huko Wisconsin waliendesha kumkaribisha mtoto wao sio mama tu alikuwa na usiku uliokumbwa na visanga bali baba pia alishiriki kwa njia ambayo hakuwa ameitarajia.

Kujifungua kwake April Neubauer, hakukuwa rahisi kwa sababu alikumbwa na tatizo linalofahamika kama pre-eclampsia, na mpigo wa juu wa damu, hali iliyosababisha akimbizwe chumba cha dharura cha upasuaji.

Wakati mtoto Rosalie alizaliwa tarehe Juni 26, mama yake April alikumbwa na tatizo lingine ndipo akapelekwa kwa matibabu zaidi kabla ya hata kumshika mtoto wake.

Kwa sababu ya hilo mtoto Rosalie ambaye alikuwa na uzani wa kilo 3.6 akakabidhiwa baba yake Maxamilllian.

"Muuguzi akaja na msichana wangu mrembo , tukaenda chumba cha watoto, nikaketi na kuvua shati langu ili nimkumbatie mtoto," aliiambia BBC.

Haki miliki ya picha Maxamillian Kendall Neubauer
Image caption Nilikuwa mtu wa kwanza kumnyonyesha mtoto

Muuguzi akasema kuwa walihitaj kumpa mtoto maziwa ya unga kwanza.

"Kisha muuguzi akauliza kama nitaweza kutoa titi langu nimnyonyeshe. Na mimi nikiwa mtu ambaye anapenda kujaribu mambo, nikasema mbona nisifanye hivyo"

Muuguzi akaunganisha mrija ambao ulikuwa umeunganishwa na sirinji iliyokuwa na maziwa ya unga kwa kifua chake Maxamillian.

"Sijawai kunyonyesha au hata kufikiria kwa miaka 1000 ningefanya hivyo. Ni mimi nilikuwa wa kwanza kumnyonyesha mtoto!

Haki miliki ya picha Maxamillian Kendall Neubauer
Image caption Baba akimnyonyesha mtoto

"Mama mkwe hakuamini kile alikuwa anakiona," alisema.

"Nilihisi kuwepo uhusiano wa karibu dakika ya kwanza nilimuona mtoto."

Kile alichokifanya Maxamillian kimezungumziwa vizuri baada ya kuandika alichokipitia kwenye mitandao ya Facebook na Instagram.

Wengine wamempongeza muuguzi ambaye alifanya uamuzi huo.

Haki miliki ya picha Maxamillian Kendall Neubauer
Image caption Maxamillian amesema alifanya kile kila baba mzuri anaweza kukifanya

Licha ya taarifa hiyo kusambazwa mara 30,000 na kuzua mamia ya maoni, Maxamillian anasema alifanya kile kila baba anaweza kukifanya.

Nilifanya hivyo ili niwe baba mzuri na shujaa kwa wauguzi mashujaa wa hospitali kwa kuwa wao ndio mashujaa wakubwa.

Mada zinazohusiana