Mhamiaji wa DRC akwea sanamu kubwa ya Statue of Liberty Marekani

A person is spotted sitting at the base of the Statue of Liberty in New York, 4 July 2018 Haki miliki ya picha @sarah_eyebrows/Twitter
Image caption Mkimbizi wa DRC akwea sanamu kubwa Marekani

Mwanamke aliyekwea sanamu kubwa Marekani la Statue of Liberty na kuketi yuko kuzuizini kwa mujibu wa polisi.

Watalii waliondolewa kutoka kisiwa cha Liberty kwenye bandari ya New York Jumatano wakati wa sarakasi hiyo iliyodumu masaa matatu.

Ametajwa na vyombo vya habari vya Marekani Therese Okoumou, mhamiaji wa miaka 44 kutoka DR Congo.

Bi Okoumou anaripotiwa kupinga sera za Trump zisizovumilia uhamiaji.

Mapema watu kadha walukamatwa kwa kundamana kwenye sanamu hiyo.

Wanachama wa kundi la wanaharakati Rise and Resist mapema waliweka bango kwenye sanamu hiyo.

Polisi wa bustani na idara bustani mjini New York waliitwa eneo hilo kufuatia ripoti kuwa mtu alikuwa akiikwea sanamu hiyo.

Baadaye Sarah akasema kuwa watalii walikuwa wakiondolewa

Iliwachukua polisi saa tatu kumteremsha Bi Okoumou kwa kutumia ngazi. Walisema wakuu wa mashtaka wataamua baadaye ikiwa atafunguliwa mashtaka.

Brian Glacken wa idara ya polisi ya mjini New York alisema haikuwa oparesheni rahisi.

Maandamano yamekuwa yakifanyika kote Marekani baada ya taarifa kuibuka kuwa maajenti walikuwa wamewatenganisha maelfu ya watoto wadogo kutoka kwa wazazi ambao wameingia Marekani kinyume na sheria.

Mwezi Februari waandamanaji waliweka bango kubwa lenye maandishi "Karibu wahamiajia" kwenyr sanamu hiyo.

Kutundika vifaa kwenye sanamu ya taifa, ambayo ni ishara ya Marekani kukuwakubali wahamiaji, ni marufuku nchini Marekani, kwa mujibu wa polisi wa bustani za taifa.