Mganga aliyedai kuwa na nguvu za kuzuia risasi apigwa risasi na kufariki Nigeria

Mganga aliyedai kuwa na nguvu za kuzuia risasi apigwa risasi na kufariki Nigeria Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mganga aliyedai kuwa na nguvu za kuzuia risasi apigwa risasi na kufariki Nigeria

Mganga mmoja nchini Nigeria amefariki baada ya mteja wake kujaribu iwapo ana nguvu za kuzuia risasi kuingia mwilini mwake kama alivyodai.

Chinaka Adoezuwe , 26, aliuawa baada ya kumuagiza mteja wake kumpiga risasi alipokuwa akivaa nguvu hizo za kuzuia risasi katika shingo yake.

Maafisa wa polisi katika jimbo lililopo kusini mashariki la Imo wanasema kuwa mteja huyo sasa amekamatwa kwa madai ya mauaji

Nguvu za uganga ni maarufu nchini Nigeria , ambapo waganga huombwa kuwatibu raia magonjwa tofauti.

Lakini kumekuwa na ripoti kadhaa za watu kula nguvu za kuzuia risasi na dawa.

Kijana mmoja alikuwa amemtembelea mganga huyo ili kupata nguvu za kuzuia risasi ambazo mganga huyo alimpatia, kulingana na mwanakijiji mmoja aliezungumza na gazeti la Punch.

Ili kuthibitisha kwamba nguvu hizo zinafanya kazi , alisimama na kumpatia mteja wake bunduki. Na hapo ndiposa janga likatokea!.

Mnamo mwezi Januari , muuzaji wa dawa za kienyeji alikamatwa baada ya mtu mmoja aliyedaiwa kunywa maji ya kuzuia risasi kuuawa.

Muuzaji huyo anayeishi kaskazini magharibi mwa Nigeria aliripotiwa kumhakikishia mtu huyo kwamba hatofariki atakapopigwa risasi.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii